Posts

Showing posts from April, 2018

Wazazi watakiwa kufichua watoto wenye maradhi ya moyo

Image
Na, Haji Nassor Sauti ya Mnyonge, Pemba WAZAZI na walezi wa watoto wenye maradhi ya moyo Zanzibar, wametakiwa kuwafichua watoto wao, na kuwapeleka katika kliniki za hospotali za serikali, ili kufanyiwa uchunguuzi na kisha kupatiwa matibabu ya haraka. Ushauri huo umetolewa na aliekuwa mgonjwa wa mwanzo Zanzibar kufanyiwa operesheni mbili ndani ya mwezi mmoja nchini Is-rail mwaka 1999  Arafa Abdulla Ali alipokua akizungumza na mwandishi wa habari hizi kisiwani Pemba. Alisema ugonjwa wa moyo unatibika na unapona na kurudi katika hali ya kawaida, hivyo hakuna sababu kwa wazazi au walezi kuwavundika ndani watoto wao. Alisema serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia wizara yake ya Afya, imekuwa na ushirikiano mzuri wa kimatibabu na nchi za India na Is-rail, hivyo kwa sasa wazazi hawana sababu ya kuogopa gharama za matibabu, kwa vile hilo hubebwa na nchi husika. Alieleza kuwa, yeye alifanikiwa kupona maradhi hayo ya moyo kutokana na wazazi wake, kumfikisha mapema hospitali ya Mnazi mmoja, na

Mtuhumiwa wa kosa la ubakaji aachiwa huru

Image
Na, Mwandishi Wetu, Sauti ya Mnyonge, Zanzibar BAADA ya kusota rumande kwa kipindi cha zaidi ya miezi miwili , hatimaye kijana Njile Masalu  Nchilu mkaazi wa Kifumbikai Wete , ameachiwa huru na mahakama ya mkoa wa Kaskazini Pemba. Kijana huyo aliyekuwa anatuhumiwa kwa kosa la kubaka ameachiwa huru na mahakama hiyo baada ya shahidi namba moja ambaye ndiye mwathirika wa tukio hilo kukana kufanyiwa kitendo hicho . Msichana huyo mwenye umri wa miaka 15 , amekana kufanyiwa kitendo hicho mbele ya hakimu wa mahakama hiyo Makame Mshamba Simgeni na mwendesha mashtaka wa serikali Ramadhan Suleiman Ramadhan , jambo ambalo limeifanya mahakama kuliondoa shauri hilo mahakamani hapo . Baada ya mahakama kuliondoa shauri hilo , kijana Njile aliondoka nduki kali katika viwanja wa mahakama , mithili ya wakimbiaji wa mbio za relay , huku akiwa haamini kilichotokea. Njile alikuwa anakabiliwa na tuhuma ya kumbaka msichana mwenye umri wa miaka 15 , kosa ambalo alidaiwa kwamba amelitekeleza septemba 5 mwaka 2

Wananchi Pemba walia uchakavu wa barabara

Image
Na, Haji Nassor, Sauti ya Mnyonge, Zanzibar WANANCHI wanaotumia barabara za Wambaa, Kengeja, Kangani, Tundauwa, Chambani na Pujini mkoa wa kusini Pemba, wameiomba wizara husika kuangalia uwezekano wa kuzifanyia matengenezo ya haraka barabara hizo, kabla jazijaongezeka mashimo makubwa. Walisema kwa sasa barabara hizo, zimeshaanza mashimo yenye ukubwa tofauti jambo ambalo huwapa usumbufu wakati wanapozitumia kwa shughuli zao mbali mbali. Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi kwa nyakati tofauti walisema, ni vyema kwa wizara hiyo kuwahi mapema kabla kuharibika zaidi kwa mvua zinazoendelea kunyesha. Walisema baada ya barabara hizo kutumika zaidi ya miaka saba sasa, wakati umefika wa kuzifanyia matengenezo kwa kuziba viraka haraka kabla ya kuchakaa zaidi. Mmoja katia ya wananchi hao Hassan Makame Omar wa Mwambe, alisema sasa barabara yao imeanza kurudi kwenye ubovu wa uwasili wake kutokana na kuzidiwa na mashimo. “Mashimo yameanza kuwa mingi, jambo ambalo hupata mtikisiko mkubwa wanapoku

Afariki dunia kwa kujinyonga akiwa msikitini

Image
Na, Haji Nassor, Sauti ya Mnyonge Zanzibar KIJANA mmoja  Azani Abdalla Suleiman (28)mkaazi wa Ole Mchanga Mrima Mkoa wa Kaskazini Pemba, amefariki dunia usiku wa kuamkia jana, kwa kujinyonga katika Msikiti ulipo kijiji cha Machomane Wilaya ya Chakechake mkoa wa Kusini Pemba. Akithitisha kutokea kwa tukio hilo, kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa kusini Pemba Sheihan Mohamed Sheihan alisema, tukio hilo limegundulika wakati waumini wa dini ya kiislamu, walipofika msikitini kwa ajili ya kusali sala ya alfajiri. Alieleza kuwa mara baada ya watu hao kuingia Msikitini kwa ajili ya kutekeleza ibada hiyo, ndipo walipokutana na mkasa huo na kuona maiti ya kijana huyo ikiwa inaninginia kutokana na kamba aliojifunga. Sheihan alisema taarifa walizobaini kwa haraka sana ni kwamba juzi kijana huyo alifika kwa Babu yake ambae ni Omar Hamad Bakari mkaazi wa Machomane Chake Chake na kumpatia taarifa juu ya adhama yake ya kutaka kufunga ndoa. ‘’Tumeambiwa kwamba hakukua na mafahamiano mazuri na babu yake

Waomba gharama za ‘passport’ kufutwa kwa wagonjwa wa moyo

Image
Na, Haji Nassor, Sauti ya Mnyonge, Zanzibar JUMUIYA ya watoto wenye maradhi ya moyo Zanzibar ‘OCHZ’ imesema, wakati umefika kwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ile ya Zanzibar, kukubalia ili kuondoa gharama za hati ya kusafiria “pass port” kwa wagonjwa wa moyo, kwa lengo la kuepusha kukosa kufanyiwa matibabu nje ya nchi, baada ya wafadhili kukubali kugharimia matibabu yao. Mwenyekiti wa Jumuia hiyo dk Omar Mohamed Suleiman, alisema wakati mwengine wagonjwa hao wengi wao wakiwa watoto, hupata ufadhili kutoka kwa mashirika mbali mbali ya kimataifa na watu binafsi, ingawa wapo waliokwama kwa kutokuwa na gharama za pasi ya kusafiria. Akizungumza kwenye mkutano wa siku moja kwa madaktari, wadau wa maradhi ya moyo na wanahabari uliofanyika hospitali ya Chakechake, Mwenyekiti huyo alisema, gharama ya pasi ya kusafiria imekuwa ikiwakwaza, baadhi ya wazazi wenye kipato cha chini, ingawa wakati mwengine huwa wameshapa ufadhili wa matibabu hayo. Alieleza kuwa kupitia Jumuia hiyo, w

Matukio mbalimbali ziara ya Jaji Mkuu wa Zanzibar kisiwani Pemba

Image
JAJI Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu, akiangalia kwenye kabati la mahakama ya Mwanzo Chakechake, wakati alipofika kuangali utendaji wao wa kazi, kabla ya kumaliza ziara yake ya siku nne kisiwani Pemba ambapo pia alizungumza na wafanyakazi wa mahakama hiyo WAFANYAKAZI wa Mahakama ya ardhi mkoa wa kusini Pemba, pamoja na mahakama nyengine, wakimsiliza Jaji mkuu Zanzibar Omar Othman Makungu, akizungumza nao kwa nyakati tofauti, kwenye mikutano yake ya ndani, ikiwa ni ziara yake kwenye mahakama hizo, kisiwani Pemba JAJI mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu akiwa na hakimu dhamana wa mahakama ya mwanzo Kengeja wilaya ya Mkoani Pemba, ambapo Jaji huyo alifika mahakamani hapo kuitembelea mahakama hiyo na kuzungumza na wafanyakazi wa mahakama hiyo MRAJI wa Jimbo Mahakama kuu Pemba Hussien Makame Hussien, akizungumza ndani ya Mahakama ya wilaya Konde, mbele ya Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu, wakati Jaji huyo akizungumza na wafanyakazi wa Mahakama hiyo Picha zote na Haji Nassor,

TCRA watoa somo la matumizi ya mitandao mkoani Mtwara

Image
Na Sijawa Omary,  Sauti ya Mnyonge, Mtwara WANANCHI katika halmashauri ya wilaya ya mtwara mkoani hapa wameipongeza mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa jitihada zake hasa utoaji wa elimu kwa wananchi hao juu ya matumizi sahihi ya mitandao ya simu kutokana na kuwepo kwa baadhi ya changamoto wanazokumbana nazo katika huduma hiyo. Elimu hiyo imetolewa hivi karibuni mjini mtwara na mamlaka hiyo huku waandaji wa mafunzo wakiwa ni shirika lisilokuwa la kiserikali mkoani hapa (MSOAPO) lengo likiwa kuwajengea uelewa zaidi wakazi hao ili waweze kuepukana na changamoto na kuelewa matumizi sahihi ya mitandao mbalimbali ya kijamii kupitia simu zao. Mafunzo hayo yametolewa kwa viongozi kutoka serikali za mitaa katika kata tano kwenye halmashauri hiyo na kwamba wakawe mabalozi wazuri wa kufikisha elimu hiyo ngazi ya chini lakini pia kuhakikisha wananchi wao wanakuwa na uelewa juu ya elimu hiyo. Katika washiriki hao Salum Athumani amesema, elimu hiyo imekuwa na tija kutokana wamekuwa wakikumba

Mkuu wa wilaya ahamasisha wazazi kupeleka watoto chanjo ya saratani

Image
Na Sijawa Omary Sauti ya Mnyonge, Mtwara WAZAZI  wenye watoto wa kike wenye umri wa miaka 14 wametakiwa kuhamasisha watoto wa kujitokeza kwa wingi kupata chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi ili kupunguza tatizo hilo pamoja na vifo vinavyotokana na ugonjwa huo. Mkuu wa wilaya ya Mtwara Evod Mmanda Wito huo umetolewa hivi karibuni mjini Mtwara na mkuu wa wilaya ya mtwara Evod Mmanda wakati alipokuwa akizungumza na wadau mbalimbali mkoani hapa namna ambavyo zoezi hilo la njano linafanyika huku akihamashisha jamii hiyo kujitokeza kwa wingi ili zoezi hilo liweze kufikiwa malengo husika.   “Jamii inapawa itambue kuwa saratani hii mara nyingi imekuwa ikiwakuta akina mama ambao bado wako kwenye uzazi sasa ungonjwa huu unapoacha kutibiwa na kukingwa mapema tunapoteza nguvu kazi ya taifa kiuchumi na msingi wa familia”.Amesema Mmanda Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Wedson Sichalwe amesema, uchunguzi wa saratani hutolewa bila malipo yoyote katika vituo vyao vya kutolea huduma katika mkoa huu na k

Ahukumiwa kifungo cha miaka 11 kwa kubaka na kumpa ujauzito mwanafunzi

Image
Na, Haji Nassor, Sauti ya Mnyonge, Zanzibar MAHAKAMA ya mkoa Chakechake, imemtupa chuo cha mafunzo miaka 11 kijana Yassir Mohamed Nassor miaka 19, wa Machomane, baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka na kisha kumpa ujauzito mtoto wa miaka 13. Hakimu wa mahakama hiyo Hussein Makame Hussein, alitoa adhabu hiyo, baada ya kijana huyo kupatikana na makosa mawili sambamba, ambapo kosa la kwanza la ubakaji atatumikia miaka saba (7) na kutoa fidia ya shilingi laki 600,000. Ambapo kosa hilo ni kinyume na kifungu cha 125 (1), (2) (e) na 126 (1) cha sheria no 6 ya mwaka 2004 sheria ya Zanzibar. Kosa la pili alilobainika nalo kijana huyo mbakaji, ni kumpa ujauzito mtoto huyo wa miaka 13, ambapo kinyume na kifungu cha 3 (3), (4) sheria ya kuwalinda wari na wajane no 4 ya mwaka 2005. Kosa hilo, Hakimu Hussein baada ya kuwasikiliza mashahidi tisa akiwemo Mchunguzi mkuu na mtaalamu wa vina saba DNA, mtoto mwenyewe, daktari, mpelelezi, mama mzazi ndipo alipotumia sheria na kumpeleka chuo cha mafunzo m

MSOAPO latoa somo kuhusu ukatili wa kijinsia Mtwara

Image
Na, Sijawa Omary,  Sauti ya Mnyonge, Mtwara SHIRIKA lisilokuwa la kiserikali mkoani Mtwara (MSOAPO) limewapiga msasa wananchi zaidi ya 40 kutoka halmashauri ya wilaya ya mtwara mkoani hapa katika swala zima la ukatili wa kijinsia kutokana na vitendo vya ukiukwaji wa kisheria vinavyoendelea katika jamii zao. Mafunzo hayo yamefanyika hivi karibuni mjini mtwara ambapo yameshirikisha washiriki kutoka vijiji 12 katika kata tano kwenye halmashauri hiyo (Viongozi) huku lengo likiwa ni kuwajengea uwezo wananchi hao wakiwa kama sehemu ya walimu au mabalozi katika maeneo yao. Mratibu wa mradi huo wa kuwajengea uwezo wananchi hao kutoka katika shirika hilo Mustapha Kwiyunga amesema kuwa, vitendo vya ukatili kwa kiasi kikubwa vipo katika maeneo yote mkaoni hapa ikiwemo mjini na vijijini hivyo ipo haja ya kuwahakikisha jamii inawafikia elimu hiyo ipasavyo. Amesema, kuwepo kwa mambo hayo katika jamii zao ni kutokana na watu au jamii kushindwa kutambua matendo yanayotokana na vitendo hivyo lakini pia

Ziara ya Jaji Mkuu Zanzibar mhe. Omar Othman Makungu katika picha

Image
MRAJISI wa jimbo mahakama kuu Pemba Hussein Makame Hussein, akisalimiana na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Micheweni Pemba, wakati alipofika hapo akijumuika kwenye ziara ya Jaji Mkuu Zanzibar, Omar Othman Makungu kisiwani humo MRAJISI wa Mahakama kuu Zanzibar Mohamed Ali Mohamed (kulia), akibadilishana mawazo na Mrajis wa jimbo mahakama kuu Pemba, Hussein Makame Hussein, kabla ya Jaji Mkuu kuzungumza na watendaji wa mahakama ya Mwanzo Dodeani Wingwi wilaya ya Micheweni, ikiwa ni sehemu ya ziara ya siku nne kisiwani Pemba WAFANYAKAZI wa mahakama ya mwanzo Wingwi Dodeani wilaya ya Micheweni, wakimsikiliza Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu, wakati alipofika mahakamani hapo, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku nne, kisiwani Pemba WAFANYAKAZI wa mahakama ya mwanzo Wingwi Dodeani wilaya ya Micheweni, wakimsikiliza Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu, wakati alipofika mahakamani hapo, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku nne, kisiwani Pemba JAJI Mkuu wa Zanzibar Omar

Jaji Mkuu Zanzibar awashukia mahakimu wanaonyanyasa watuhumiwa

Image
Na, Haji Nassor, Sauti ya Mnyonge, Zanzibar JAJI mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu, amewauliza mahakimu kisiwani Pemba, wamezitoa wapi sheria zinazowapa mamlaka ya kuwalazimisha watuhumiwa, kuwa na wafanyakazi wa serikali au barua za masheha kama kigezo  wanapoomba dhamana dhidi ya kesi zinazowakabili. Alisema anashangaa kuona baadhi ya mahakimu, kuwawekea masharti magumu watuhumiwa, kwa lengo la kutafuta sababu ya kuwapelekea rumande, jambo ambalo sio sahihi maana huko sio kwahali kwema kwa kukaa mwanadamu. Jaji Mkuu huyo alieleza hayo, kwa nyakati tofauti, walipokuwa akizungumza na watendaji wa mahakama za mwanzo Wingwi, Konde na Wete, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku nne kisiwani Pemba. Alisema lazima mahakimu waelewa kuwa, kumpeleka mtuhumiwa rumande ni hatua ya mwisho, na sio iwe ndio kipaumbele chao, kwa kuwekea masharti magumu au kima kikubwa cha fedha taslimu. Alieleza kuwa, yeye binafsi hajaona popote kwenye sheria, kuwa mtuhumiwa anatakiwa ili kutimiza masharti, kwamb

Walengwa 175 wa TASAF wawanufaisha wakulima wa mpunga 230

Image
Na, Haji Nassor Sauti ya Mnyonge, Pemba WALENGWA 175 waliomo kwenye mpango wa kunusuru kaya maskini unaoendeshwa na TASF III, shehia ya Kendwa wilaya ya Mkoani Pemba, wanatarajiwa kuwanufaisha wakulima wa mpunga 230 wa bode la Egeyani, kuwa na kilimo cha uhakika kuanzia msimu ujao.  Walengwa hao wapo kwenye bonde hilo kwa sasa wakiendelea na kazi ya kuchimba misingi ya kisasa, ambayo italiwezesha bonde hilo kuondokana na mfumo wa ziwa ambapo uwingi wa maji uliokuwepo kwa muda mrefu haukuwa ukiwanufaisha wakulima hao. Mwandishi wa habari hizi, alishushuhudia kazi ya kuchimba misingi kwenye bonde hilo zikiendelea kwa kasi, ambapo miundombinu inayowekwa kwenye bonde hilo, sasa itakinga uwepo wa maji ya bahari. Baadhi ya watendaji kazi kwenye bonde hilo, walisema eneo hilo limekuwa haliwapi mfumo mzuri wakulima kutokana na kujaa maji na kufanyika ziwa, lenye kina kirefu na wakati mwengine hata kuingia maji ya bahari. Walisema kazi wanayoifanya wao kupitia mpango wa kunusuri kaya maskini, i

Sita wapotea katika mazingira tatanishi wilayani Wete

Image
Na Mwandishi Wetu, Sauti ya Mnyonge, Zanzibar kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba Haji Khamis Haji VIJANA sita wakaazi wa kijiji cha Mitambuuni Mtambwe wilaya ya Wete, Mkoa wa kaskazini Pemba hawajulikani walipo baada ya kutokweka tokea April 4 mwaka huu. Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa badhi ya wanananchi wa maeneo hayo, walisema watu hao walivaamiwa na kundi la watu zaidi ya 15 waliokuwa na silaha na kuwachukua ambapo hawajui wapo walipopelekwa.  Vijana walitoweka usiku wa huo  ni Thuwein  Nassor (30) Khamis Abdalla Matar (22) Juma Kombo (17) Said Shanani (16) Khalid Khamis (29) na Abdalla Khamis (19) Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo walisema kuwa, wakiwa wamelala ghafla walisikia mlio wa gari ukingia kwenye kijiji chao huku watu waliovalia viatu vya buti na wakiwa wamebeba silaha za moto walishuka na kuvunja milango kwa baadhi ya nyumba. Mmoja miongoni mwa wakaazi wa Mitambuuni aliyejitambulisha kwa jina la Said Nassor Hemed alisema kabla ya kutokea kutio hilo la ut

Daktari ajitolea kutibu watoto wa wasiojiweza kwa pesa zake mwenyewe

Image
Na, Haji Nassor, Sauti ya Mnyonge, Pemba MKUU wa Kituo cha Afya kisiwa cha Makoongwe wilaya ya Mkoani Pemba, Rajab Juma Seif, ameamua kununua asali kwa fedha zake, ili kuwasaidia watoto wenye kuumwa na kifu kwa muda mrefu. Alisema, aliamua kufanya hivyo ili kuwasaidia watoto na hasa ambao wazee wao hawana uwezo, ili kuponya kifua kwa pale wanapohitaji matumizi ya dawa hiyo. Akizungumza na mwandishi wa habari hizi hospitalini hapo, alisema zipo dawa ambazo hushabihiana na asali matibabu yake, ambapo pia kama mgonjwa akikosa dawa husika akitumia asali anaweza kupona na ndio maana ameamua kuwa nayo. Alisema asali hiyo huwauzia wanaohitaji kati ya shilingi 2,500 hadi shilingi 3,000 na wale wasio kuwa na uwezo kabisa wakati mwengine huwapa bila ya malipo yoyote. Mkuu huyo wa Kituo cha Afya cha kisiwa cha Makoongwe, alisema sio wote wanaoumwa kama wanauwezo wa kununua dawa zinazokosekana hospitali, na ndio maana ameaandaa utaratibu huo, ikiwa ni njia ya kuwasaidia wananchi. “Wapo watoto wame

Mkuu wa Wilaya asikitishwa na uvunaji miti kiholela

Image
Na, Florence Sanawa, Sauti ya Mnyonge, Mtwara Wakati dunia ikihamasisha utunzaji wa mazingira Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Evod Mmanda amesikitishwa na kasi ya uvunaji holela wa msitu huku akiitaka jamii kufuata sheria za misitu. Kauli hiyo ameitoa juzi wakati wa maadhimisho ya upandaji miti kiwilaya uliofanyika katika kijiji cha Ndumbwe Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara ambapo alisema sema kuwa kasi ya ukataji wa miti ni kubwa kuliko upandaji hali ambayo inaongeza tishio la uharibifu wa mazingira.  “Uvunaji holela lazima uangaliwe hatuwezi kukaa kimya na kuona watu wana kata miti hovyo bila kufuata sheria tena wengine wanatumia wanatumia ile mashine ya kukatia ‘chenisor’ ni marufuku sheria za misitu zipo zifanyekazi………. “Suala la kupanda miti ni suala ambalo linazungumziwa medani za kimataifa hii inatokana na uharibifu wa mazingira ambao umekuwa ukijitokeza kwa kasi tukishirikiana tunaweza kulinda mazingira yetu” “Katika ngazi ya familia mti una faida ya kivuli sisi kauli mbiu yetu tunataka

Wapinga mkutano mkuu wa dayosis hadi mgogoro utakapomalizika

Na, Florence Sanawa Sauti ya Mnyonge, Mtwara WAZEE wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) Usharika wa Mtwara wamepinga kufanyika kwa Mkutano Mkuu wa Sinodi (Dayosisi) kabla ya kumaliza mgogoro  uliopo katika kanisa hilo dhidi ya askofu wa jimbo hilo Lucas Judah Mbedule uliodumu kwa zaidi ya miaka miwili sasa. Kanisa hilo liliingia katika mgogoro baada ya kumtilia mashaka na kumtuhumu Askofu huyo kuwa na matumizi mabaya ya fedha  na kujimilikisha mali na viwanja vya kanisa hilo kinyume na taratibu za kanisa. Akitoa tamko hilo wakati wa ibada leo mmoja wa waumini wa kanisa hilo aliyeteuliwa na wazee Steven Macha alisema kuwa  takribani miaka miwili sasa kanisa hilo limekuwa na  mvutano kati ya washirika hao wanaohitaji kuondolewa kwa Askofu huyo. Alisema kuwa askofu huyo amekuwa akitenda mambo yasiyozingatia mafundisho ya kikristo kwa kwenda kinyume na madhabahu na kusababisha kuvurugwa kwa utaratibu wa heshima ya cathedral na kanisa kwa ujumla. Macha alisema kuwa mkutano huo wa Sinod

Mbunge akabidhi gari la kubebea wagonjwa kituo cha afya Dinyecha

Image
Na, Florence Sanawa, Sauti ya Mnyonge, Mtwara MBUNGE wa Jimbo la Nanyamba Abdallah Chikota (CCM) amewataka watumishi wa Kituo cha Afya Dinyecha kutunza gari walilopewa na serikali ili liweze kuwasaidia kutatua changamoto ya usafiri wanapohitaji kumsafirisha mgonjwa  kwenye hospitali kubwa pale anapozidiwa. Akikabidhi gari hilo kwa Mganga Mfawidhi wa Kituo hicho Dk. Nyangocho Nyabaiga, Mbunge huyo alisema kuwa ujio wa gari hilo utasaidia wakazi hao na kuwarahisishia usafiri pale wanapopata mgonjwa kutokana na halmashauri hiyo kuwa na kituo kimoja cha afya. Alisema kuwa hatua hiyo itawasukuma kukamilisha ujenzi wa vituo vingine vya afya viwili ambapo vikikamilika halmashuri hiyo itakuwa na vituo vitatu vya afya hivyo kuwaondolea wananchi hao usumbufu wa kutafuta huduma ya afya ndani ya halmashauri hiyo. “Unajua hawa wananchi walikuwa wakipata adha ya kusafiri umbali mrefu tena kwa magari ya kukodi ama pikipiki ili kuweza kuwahisha wagonjwa katika vituo vya afya katika wilaya za jirani  t

Mamlaka ya Bandari Mtwara yaipiga tafu hospitali ya Rufaa Mtwara

Image
Na, Florence Sanawa, Sauti ya Mnyonge, Mtwara MAMLAKA ya Bandari Tanzania Mkoa wa Mtwara  imewakumbuka wanyonge Hospitali ya Rufaa Ligula kwa kutoa shuka 100 zenye thamani ya zaidi ya shilingi 1,300,000 ambapo inapelekea Hospitali hiyo kuwa na upungufu wa shuka 800 tu kwa sasa. Akipokea shuka hizo Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo Dickson Sahini alisema kuwa hospitali hiyo ina vitanda 248 ambapo vinatakiwa kuwa na shuka 8 kwa kila kitanda hali ambayo inakuwa ngumu kutokana na uhaba uliopo hospitlaini hapo. hospitali hiyo ilikuwa na upungufu wa shuka 900 ambapo baada ya kupata hizo wanaupungufu wa shuka 800 ili kupata shuka 8 kwa kila kitanda kama taratibu zinavyotakiwa kuwa. “Tunayo pia changamoto ya uboreshaji wa majengo ambayo hivi sasa ni chakavu, tuna tatizo kubwa la uhana wa  vifaa tiba, vifaa vishirikishi ikiwemo mashine ya kufulia” alisema Sahini Kwa upande wake Mkuu wa Bandari Mkoa wa Mtwara Nelson Mlali alisema kuwa mamlaka hiyo imeamua kutoa shuka hizo ili kuweza kuisai

TASAF yahifadhi chanzo cha maji Mkiang’ombe Pemba

Image
Na, Haji Nassor, Sauti ya Mnyonge, Pemba WANANCHI 250 wa kijiji cha Mkiang’ombe shehia ya Tondooni wilaya ya Micheweni kisiwani Pemba, sasa watakuwa na uhakika wa kutumia maji yasiyochanganyika na ya bahari, kama ilivyokuwa nusu karne iliopita, baada ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania, awamu ya tatu (TASAF III), kukijengea kianzio hicho. ENEO la kianzio cha maji kilichopo kijiji cha Mkiang’ombe shehia ya Tondooni wilaya ya Micheweni Kisiwani Pemba, ambapo kwa sasa kimehifadhiwa na TASAF III, na kuzuia uwezekano wa kuingia maji ya baharai kama ilivyokuwa miaka 50 iliopita, ambapo mradi huo umeibuliwa na walengwa waliomo kwenye mpango wa kunusuru kaya maskini shehiani humo Awali wananchi  wa eneo hilo, walikuwa wanatumia maji ya matumizi ya kawaida yanayochanganyika na ya bahari, kutokana na kianzio chao kilichopo pembezoni mwa ufukuwe, kuingiliwa na maji ya bahari wakati yanapokuja juu. Sheha wa shehia hiyo Abdalla Bakar Dawa, alisema wananachi wake walikuwa wakihangaika kwa nusu k

Shirika la Umeme Zanzibar lakusanya bilioni 5 kwa siku 150 kwa wateja wake

Image
Na, Haji Nassor, Sauti ya Mnyonge, Zanzibar SHIRIKA la Umeme Zanzibar ZECO tawi la Pemba, lenye wastani wa wateja 31,313 limeshakusanya shilingi bilioni 5 na milioni 183 kwa kip indi cha miezi mitano, ilioanzia mwaka jana, hadi mwezi Febuari mwaka huu. Taarifa kutoka ZECO zinaeleza kuwa, idadi ya wateja imekuwa ikiongezeka siku hadi siku, kutokana na huduma bora na imara wanazozitoa kwa wananchi na wakati wowote wananchi 200 waliobakia katika mita za zamani, watahamishiwa mita za kisasa. Meneja wa shirika hilo Pemba, Mohamed Juma Othman alisema wamekuwa wakikusanya fedha zenye kiwango toafuti kutokana na mahitaji ya wateja wao kwa kila mwezi. Alisema, kwa mfano katika mwezi wa Oktoba Shirika lilikusanya wastani wa shilingi milioni 961, ambapo mwezi Novemba kwa mikoa yote miwili ya Pemba lilikusanya shilingi milioni 975, ingawa mwezi Disemba mwaka jana, liliongeza na kukusanya shilingi bilioni 1.105. Aidha katika kipindi cha miezi miwili iliopita ndani ya mwaka huu wa 2018 na kwenye mwe