Mkuu wa wilaya ahamasisha wazazi kupeleka watoto chanjo ya saratani

Na Sijawa Omary
Sauti ya Mnyonge, Mtwara

WAZAZI  wenye watoto wa kike wenye umri wa miaka 14 wametakiwa kuhamasisha watoto wa kujitokeza kwa wingi kupata chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi ili kupunguza tatizo hilo pamoja na vifo vinavyotokana na ugonjwa huo.

Mkuu wa wilaya ya Mtwara Evod Mmanda
Wito huo umetolewa hivi karibuni mjini Mtwara na mkuu wa wilaya ya mtwara Evod Mmanda wakati alipokuwa akizungumza na wadau mbalimbali mkoani hapa namna ambavyo zoezi hilo la njano linafanyika huku akihamashisha jamii hiyo kujitokeza kwa wingi ili zoezi hilo liweze kufikiwa malengo husika.  

“Jamii inapawa itambue kuwa saratani hii mara nyingi imekuwa ikiwakuta akina mama ambao bado wako kwenye uzazi sasa ungonjwa huu unapoacha kutibiwa na kukingwa mapema tunapoteza nguvu kazi ya taifa kiuchumi na msingi wa familia”.Amesema Mmanda

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Wedson Sichalwe amesema, uchunguzi wa saratani hutolewa bila malipo yoyote katika vituo vyao vya kutolea huduma katika mkoa huu na kutokana na ukubwa wa tatizo serikali imefanya jitihada kubwa kuhakikisha tatizo la saratani linamalizika ambapo watoto zaidi ya elfu 16 wanatarajia kupatiwa chanjo hiyo mkoani hapa.

Kwa upande wao viongozi wa dini akiwemo askofu Lucas Mbedule kutoka kanisa la kiinjili la kilutheli Tanzania Dayosisi ya  Kusini mashariki Mtwara (KKKT)  amesema, kwa nafasi yao wameipongea serikali kwa hatua hiyo mzuri kuhakikisha inapambana na tatizo hilo ambalo hadi kufikia hivi sasa wameshapoteza ndugu zao wengi.

Naye ustadhi Hassan Mbwago katibu wa baraza kuu la waislaamu wilayani mtwara (BAKWATA) amesema, kitendo cha serikali kushirikisha viongozi wa dini ni jambo jema kutokana tatizo hilo ni lao wote na kwa sehemu yao watahakikisha linaenda sawa sawa.

Comments

Popular posts from this blog

Wananchi wajenga wodi baada ya kuchoshwa na kujifungulia sakafuni

Sita wapotea katika mazingira tatanishi wilayani Wete

Jaji Mkuu Zanzibar awashukia mahakimu wanaonyanyasa watuhumiwa