Ziara ya Jaji Mkuu Zanzibar mhe. Omar Othman Makungu katika picha
MRAJISI wa jimbo mahakama kuu Pemba Hussein Makame Hussein, akisalimiana na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Micheweni Pemba, wakati alipofika hapo akijumuika kwenye ziara ya Jaji Mkuu Zanzibar, Omar Othman Makungu kisiwani humo
MRAJISI wa Mahakama kuu Zanzibar Mohamed Ali Mohamed (kulia), akibadilishana mawazo na Mrajis wa jimbo mahakama kuu Pemba, Hussein Makame Hussein, kabla ya Jaji Mkuu kuzungumza na watendaji wa mahakama ya Mwanzo Dodeani Wingwi wilaya ya Micheweni, ikiwa ni sehemu ya ziara ya siku nne kisiwani Pemba
WAFANYAKAZI wa mahakama ya mwanzo Wingwi Dodeani wilaya ya Micheweni, wakimsikiliza Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu, wakati alipofika mahakamani hapo, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku nne, kisiwani Pemba
WAFANYAKAZI wa mahakama ya mwanzo Wingwi Dodeani wilaya ya Micheweni, wakimsikiliza Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu, wakati alipofika mahakamani hapo, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku nne, kisiwani Pemba
JAJI Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu, akizungumza na watendaji wa Mahakama ya Mwanzo Wingwi Dodeani, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku nne kisiwani Pemba
JAJI mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu, akiwa na watendaji wa mahakama ya wilaya Konde, akilitembelea aneo la mahakama hiyo, kwenye ziara yake ya siku nne kisiwani Pemba
WATENDAJI wa mahakama ya wilaya Konde, wakimsikiliza Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu, wakati alipokuwa akizungumza nao, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku nne kisiwani Pemba,
JAJI mkuu wa Zanzibar Omar Othman Mkungu, akiwa na Mrajisi na manaibu wa warajisi wa Mahakama Kuu Zanzibar, wakisikiliza taarifa ya utendaji kazi, iliosomwa na hakimu wa mahaka ya ardhi, mkoa kasakazini Pemba
ENEO la soko kuu la kisasa la mjini Wete Pemba, ambalo limejumuisha egesho kuu la gari za abiria, ambapo wananchi na wamiliki wa gari wakiendelea kulitumia
Picha zote na Haji Nassor wa Sauti ya Mnyonge, Zanzibar
Comments
Post a Comment