Mkuu wa Wilaya asikitishwa na uvunaji miti kiholela

Na, Florence Sanawa,
Sauti ya Mnyonge, Mtwara

Wakati dunia ikihamasisha utunzaji wa mazingira Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Evod Mmanda amesikitishwa na kasi ya uvunaji holela wa msitu huku akiitaka jamii kufuata sheria za misitu.

Kauli hiyo ameitoa juzi wakati wa maadhimisho ya upandaji miti kiwilaya uliofanyika katika kijiji cha Ndumbwe Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara ambapo alisema sema kuwa kasi ya ukataji wa miti ni kubwa kuliko upandaji hali ambayo inaongeza tishio la uharibifu wa mazingira.

 “Uvunaji holela lazima uangaliwe hatuwezi kukaa kimya na kuona watu wana kata miti hovyo bila kufuata sheria tena wengine wanatumia wanatumia ile mashine ya kukatia ‘chenisor’ ni marufuku sheria za misitu zipo zifanyekazi……….

“Suala la kupanda miti ni suala ambalo linazungumziwa medani za kimataifa hii inatokana na uharibifu wa mazingira ambao umekuwa ukijitokeza kwa kasi tukishirikiana tunaweza kulinda mazingira yetu”

“Katika ngazi ya familia mti una faida ya kivuli sisi kauli mbiu yetu tunataka kupanda miti lakini ya mikorosho ndio maana kituo cha utafiti naliendele kimeendelea kufanya tatifi mbalimbali ili tuweze kupanda miti ya mikorosho bora zaidi” alisema Mmanda

Nae Mkurugenzi wa Halmashauri ua Wilaya ya Mtwara Omari Kipanga alisema kuwa zoezi hilo litapewa kipaumbele sambasamba na kusimamia sheria ili kulinda mazingira.

 “Unajua jamii inaelewa nini maana ya utunzaji wa mazingira lakini inavunja sheria sasa tutasimama imara ili tuhakikishe kuwa kila sheria ya misitu inayovunjwa hatua zinachukuliwa kwa kushirikiana na wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS)” alisema Kipanga

Hata hivyo, TFS kwa mwaka 2016/2017 na 2017/2018 imepanda miche ya mitiki 13200 katika eneo lenye ukubwa wa hekta 12.0 katika wilaya hiyo huku Tfs kwa kushirikiana na idara ya kilimo wilayani humo kuanzia Julai 2017 hadi machi 2018 imefanikiwa kupanda miti takribani 594,879 ya aina mbalimbali ili kuendelea kuhifadhi mazingira.

Comments

Popular posts from this blog

Wananchi wajenga wodi baada ya kuchoshwa na kujifungulia sakafuni

Sita wapotea katika mazingira tatanishi wilayani Wete

Jaji Mkuu Zanzibar awashukia mahakimu wanaonyanyasa watuhumiwa