Matukio mbalimbali ziara ya Jaji Mkuu wa Zanzibar kisiwani Pemba
JAJI Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu, akiangalia kwenye kabati la mahakama ya Mwanzo Chakechake, wakati alipofika kuangali utendaji wao wa kazi, kabla ya kumaliza ziara yake ya siku nne kisiwani Pemba ambapo pia alizungumza na wafanyakazi wa mahakama hiyo
WAFANYAKAZI wa Mahakama ya ardhi mkoa wa kusini Pemba, pamoja na mahakama nyengine, wakimsiliza Jaji mkuu Zanzibar Omar Othman Makungu, akizungumza nao kwa nyakati tofauti, kwenye mikutano yake ya ndani, ikiwa ni ziara yake kwenye mahakama hizo, kisiwani Pemba
JAJI mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu akiwa na hakimu dhamana wa mahakama ya mwanzo Kengeja wilaya ya Mkoani Pemba, ambapo Jaji huyo alifika mahakamani hapo kuitembelea mahakama hiyo na kuzungumza na wafanyakazi wa mahakama hiyo
MRAJI wa Jimbo Mahakama kuu Pemba Hussien Makame Hussien, akizungumza ndani ya Mahakama ya wilaya Konde, mbele ya Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu, wakati Jaji huyo akizungumza na wafanyakazi wa Mahakama hiyo
Picha zote na Haji Nassor,
Sauti ya Mnyonge, Zanzibar
Comments
Post a Comment