Sita wapotea katika mazingira tatanishi wilayani Wete

Na Mwandishi Wetu,
Sauti ya Mnyonge, Zanzibar

kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba Haji Khamis Haji
VIJANA sita wakaazi wa kijiji cha Mitambuuni Mtambwe wilaya ya Wete, Mkoa wa kaskazini Pemba hawajulikani walipo baada ya kutokweka tokea April 4 mwaka huu.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa badhi ya wanananchi wa maeneo hayo, walisema watu hao walivaamiwa na kundi la watu zaidi ya 15 waliokuwa na silaha na kuwachukua ambapo hawajui wapo walipopelekwa.

 Vijana walitoweka usiku wa huo  ni Thuwein  Nassor (30) Khamis Abdalla Matar (22) Juma Kombo (17) Said Shanani (16) Khalid Khamis (29) na Abdalla Khamis (19)

Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo walisema kuwa, wakiwa wamelala ghafla walisikia mlio wa gari ukingia kwenye kijiji chao huku watu waliovalia viatu vya buti na wakiwa wamebeba silaha za moto walishuka na kuvunja milango kwa baadhi ya nyumba.

Mmoja miongoni mwa wakaazi wa Mitambuuni aliyejitambulisha kwa jina la Said Nassor Hemed alisema kabla ya kutokea kutio hilo la utekwaji wa watu hao, siku za  nyuma kijijini kwao  kulikua na mtindo wa kuingia gari mpya katika maeneo yao zikiwa na tinted na kuanza  kuduruduru kwa taratibu.

“Zilikua zinakuja gari tofauti tukaanza kupatwa na wasiwasi tukaamua tuwasimamishe kuwauliza lakini hawasimami , hatukuweza kuwajua ni akina nani,” alisema Hemed.

Alieleza kuwa, siku ya watu hao kuchukuliwa, walikuja watu hao kijijini kwao kisha kwenda moja kwa moja katika nyumba ya mdogo wake “Thuwein Nassor Hemed” akiwa amelala na mkewe  walimwita kwa jina lake kisha kusema kuwa wao ni maafisa wa kusachi karafuu huku wakimtaka atoke nje,

Amesema baada ya kutoka , mdogo wake walimchukua na mpaka leo hii hajuulikani alipo na hakuna mawasiliano yoyote.

Shanani Mohamed Saleh alisema watu hao hawakuwa wamevalia sare za aina yoyote hile, hivyo alishindwa kuwatambua ni akina nani inagwa aliona wamebeba silaha alizodai kuwa za moto.

“Walikuja na kuwachukua vijana wenzetu hatujui wapi wamewapeleka hadi sasa na taarifa hizi pia tumeshatoa jeshi la polisi kwa uchunguzi zaidi,”alisema Saleh.

Suleiman Nassir  alisema , yeye aliwaona lakini hakuweza kujua sura zao hata mmoja kutokana na woga aliokua nao alilazimika kujificha ili kujiunuru.

Sheha wa shehia ya Mtambwe kusini Othman Ali Khamis, alithibitisha kuwa wananchi wake hao sita hawapo katika maeneo yake, na kusema kuwa taarifa hizo alifikishiwa na wananchi.

Alisema, kama ni ukaguzi wa uliyofanyika yeye haujui maana angeshirikishwa lakini hakuna na taarifa hizo juu ya ukaguzi wa aina hiyi uliopelekea vijana wake kutekwa.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi  kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba Haji Khamis Haji alisema Jeshi hilo limepokea taarifa kutoka kwa wananchi na kwa sasa wameanza kuzifanyia kazi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ambae pia ni Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Omar Khamis Othmani alisema anasikitishwa na taarifa za matukio ya aina hio, akidai si miongoni mwa matukio yaliozoleka katika Mkoa wake.

Alisema ameagiza Jeshi la Polisi kuchunguza kwa kina tukio hilo na hatimae kubaini nani wamehusika juu hali hiyo ndani ya mkoa wake.

“Inawezekana watu wenye nia mbaya na Mkoa wetu wamekuja kuvamia na kufanya tukio hili, kwa makusudi ili kutuchafua lakini hatutakubaliani nalo,” alisema.

Hata hivyo Mkuu huyo wa Mkoa wamewataka wananchi wa eneo hilo kuendelea kuwa wastahamilivu huku Jeshi la Polisi na vyombo vyengine vinaendelea kufanyakazi zake.

Gari zilizoonekana zikitembea katika maeneo hayo na ndizo zinazotuhumiwa katika tukio hilo, wananchi walifanikiwa kunasa namba za baadhi ya gari hizo ni pamoja na  Prado Z 941 EG, nyengine ni Z 229 EQ, na nyengine hazikuweza kupatikana ambapo pia zilikuwepo RV4 nne na Fuso moja.

Hili ni tukio la kwanza katika mwaka huu kutokea kwa vijana kutekwa na watu wasiofamaika, ingawa maka jana Mkoa wa kusini kulichukuliwa vijana wawili na polisi wa vyuo vya mafunzo.a

Comments

Popular posts from this blog

Wananchi wajenga wodi baada ya kuchoshwa na kujifungulia sakafuni

Jaji Mkuu Zanzibar awashukia mahakimu wanaonyanyasa watuhumiwa