Mbunge akabidhi gari la kubebea wagonjwa kituo cha afya Dinyecha
Na, Florence Sanawa,
Sauti ya Mnyonge, Mtwara
MBUNGE wa Jimbo la Nanyamba Abdallah Chikota (CCM) amewataka watumishi wa Kituo cha Afya Dinyecha kutunza gari walilopewa na serikali ili liweze kuwasaidia kutatua changamoto ya usafiri wanapohitaji kumsafirisha mgonjwa kwenye hospitali kubwa pale anapozidiwa.
Akikabidhi gari hilo kwa Mganga Mfawidhi wa Kituo hicho Dk. Nyangocho Nyabaiga, Mbunge huyo alisema kuwa ujio wa gari hilo utasaidia wakazi hao na kuwarahisishia usafiri pale wanapopata mgonjwa kutokana na halmashauri hiyo kuwa na kituo kimoja cha afya.
Alisema kuwa hatua hiyo itawasukuma kukamilisha ujenzi wa vituo vingine vya afya viwili ambapo vikikamilika halmashuri hiyo itakuwa na vituo vitatu vya afya hivyo kuwaondolea wananchi hao usumbufu wa kutafuta huduma ya afya ndani ya halmashauri hiyo.
“Unajua hawa wananchi walikuwa wakipata adha ya kusafiri umbali mrefu tena kwa magari ya kukodi ama pikipiki ili kuweza kuwahisha wagonjwa katika vituo vya afya katika wilaya za jirani tunaamini kuwa kukamilika kwa kituo hicho na kupata gari kutatatua changamoto hiyo ilikuwa ikiwakabili kwa muda mrefu” alisema Chikota
Akipokea gari hilo Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Dinecha Dk. Nyangocho Nyabaiga alisema kuwa kupokelewa kwa gari hilo kutaongeza wagonjwa katika kituo hicho hivyo kuiomba serikali kuongeza watumishi kuwepo 11 kutokana na uchache uliopo hospitalini hapo ambapo wanatakiwa wawe 55.
Alisema kuwa ujio wa gari hilo litasaidia wagonjwa ambao watatakiwa kwenda kutibiwa katika hosptali kubwa kwa urahisi na kuwawahisha hatua ambayo itapunguza tatizo la vifo vitokanavyo na tatizo la usafiri ambalo lilikuwa likiwakabili kwa wakati huo.
Kwa upande wa wananchi wa kata hiyo Asha Ndauka mkazi wa Kijiji cha Chitondola alisema kuwa kwa kiasi kikubwa usafiri huo utawasaidia wanawake wajawazito ambao walikuwa wakitaabika hasa wanapotakiwa kwenda kupata matibabu katika hospitali kubwa.
“Ujio wa hili gari utasaidia wengi lakini zaidi itasaidia wamama wajawazito ambao awali waikuwa wanalazimika kutumia bodaboda ili kuwahishwa hospitali………..
“Wakati mwingne unachelewa kufika kutokana na usafiri hali ambayo ilipelekea watu wengi kufariki hasa wamama wajaawazito ujio wa hili gari utapunguza adha wanazopata wamama wa halmashauir hiyo” alisema Ndauka
Nae Zainab Mankala mkazi wa kata ya Dinecha alisema kuwa ujio wa gari hilo umepokelewa kwa furaha kubwa na wakazai hao jambo ambalo litawasaidia kuwaondoa katika adha kubwa waliyokuwa wakipata awali.
”Kwetu ilikuwa adhabu kubwa unapokuwa na mgonjwa na amezidiwa unalazimika kutatufa usafiri mwenyewe lakini ujio hili gari utatusaidia kwa kiasi kikubwa hata tunapopata wagonjwa tutaweza kuwahisha hospitlini…….
“Wakati mwingine uchungu ukimpata mama na akawa na shida tulikuwa na pata wakati mgumu kumuwahisha hospitalini kwakuwa tulikuwa tunatumia usarifi wa pikipiki hali ambayo ilikuwa inasababisha sisi kuwapoteza ndugu zetu kwakukosa huduma kwa wkati.” Alisema Mankala
Comments
Post a Comment