TCRA watoa somo la matumizi ya mitandao mkoani Mtwara
Na Sijawa Omary,
Sauti ya Mnyonge, Mtwara
WANANCHI katika halmashauri ya wilaya ya mtwara mkoani hapa wameipongeza mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa jitihada zake hasa utoaji wa elimu kwa wananchi hao juu ya matumizi sahihi ya mitandao ya simu kutokana na kuwepo kwa baadhi ya changamoto wanazokumbana nazo katika huduma hiyo.
Elimu hiyo imetolewa hivi karibuni mjini mtwara na mamlaka hiyo huku waandaji wa mafunzo wakiwa ni shirika lisilokuwa la kiserikali mkoani hapa (MSOAPO) lengo likiwa kuwajengea uelewa zaidi wakazi hao ili waweze kuepukana na changamoto na kuelewa matumizi sahihi ya mitandao mbalimbali ya kijamii kupitia simu zao.
Mafunzo hayo yametolewa kwa viongozi kutoka serikali za mitaa katika kata tano kwenye halmashauri hiyo na kwamba wakawe mabalozi wazuri wa kufikisha elimu hiyo ngazi ya chini lakini pia kuhakikisha wananchi wao wanakuwa na uelewa juu ya elimu hiyo.
Katika washiriki hao Salum Athumani amesema, elimu hiyo imekuwa na tija kutokana wamekuwa wakikumbana na changamoto ikiwemo kutapeliwa, kuibiwa simu zao na kushindwa njia sahihi ya kupata msaada wa haraka makosa ya utumaji wa pesa, tatizo la mtandao katika maeneo yao na kupitia elimu hiyo atakuwa balozi na umakini katika hayo.
“Neti kwetu inakuja lakini siyo kwa kasi ukianagalia muda mwingine huwezi kupata mtandao vizuri maana unaweza kupata neti mara moja halafu inakatika lingine nililojifunza kumpa mtu namba ta siri ili akanitolee pesa kumbe siyo sahihi na ni elimu tosha kwangu”, Alisema Athumani
Kaimu meneja wa mawasiliano na mahusiano ya mamlaka ya mawasiliano Tanzania Mabel Masasi amesema, mafunzo kwa viongozi hao ni kwamba waweze kutambua namna ya kutumia tekinolojia ya mawasiliano kutekeleza utawala bora ambapo wameangalia tekinolojia hiyo kuwa inaweza kuchangia utawala bora.
Mratibu wa shirika hilo Mustapha Kwiyunga amesema, elimu hiyo kwa viongozi hao ni kutokana na kipindi kilichopo hivi sasa kwa matumizi ya mitandao hivyo wanapaswa kujua faida na hasara zinatokana na tekinolojia lakini pia kuweza kupata habari na kufanya tafiti mbalimbali kupitia simu zao.
Comments
Post a Comment