MSOAPO latoa somo kuhusu ukatili wa kijinsia Mtwara



Na, Sijawa Omary, 
Sauti ya Mnyonge, Mtwara

SHIRIKA lisilokuwa la kiserikali mkoani Mtwara (MSOAPO) limewapiga msasa wananchi zaidi ya 40 kutoka halmashauri ya wilaya ya mtwara mkoani hapa katika swala zima la ukatili wa kijinsia kutokana na vitendo vya ukiukwaji wa kisheria vinavyoendelea katika jamii zao.

Mafunzo hayo yamefanyika hivi karibuni mjini mtwara ambapo yameshirikisha washiriki kutoka vijiji 12 katika kata tano kwenye halmashauri hiyo (Viongozi) huku lengo likiwa ni kuwajengea uwezo wananchi hao wakiwa kama sehemu ya walimu au mabalozi katika maeneo yao.

Mratibu wa mradi huo wa kuwajengea uwezo wananchi hao kutoka katika shirika hilo Mustapha Kwiyunga amesema kuwa, vitendo vya ukatili kwa kiasi kikubwa vipo katika maeneo yote mkaoni hapa ikiwemo mjini na vijijini hivyo ipo haja ya kuwahakikisha jamii inawafikia elimu hiyo ipasavyo.

Amesema, kuwepo kwa mambo hayo katika jamii zao ni kutokana na watu au jamii kushindwa kutambua matendo yanayotokana na vitendo hivyo lakini pia wengine hufanya huku wakiwa wanajua kuwa ni vitendo vibaya lakini kwa makusudi wanaamua kufanya hivyo.

Hata hivyo wameona eneo kubwa katika hilo ni elimu hiyo kwa jamii lakini pia kumekuwa na changamoto katika mashirika mengi au wadau mbalimbali kwa kuwa na jitihada za utoaji wa elimu hiyo na badala yake kutokea kwa kesi nyingi za matukio hayo huku akiomba serikali na mashirika hayo kuwa na jitihada za makusudi juu ya utoaji wa elimu hiyo.

Hata hivyo mwakilishi wa dawati la jinsi la kutoka jeshi la polisi wilaya ya mtwara Salma Abdallah amesema, majukumu yao ni kuhakikisha familia hazitofautiani au kutengana ambapo wamekuwa wakipatanisha na kuwaweka watu katika hali ya maelewano kwa kuwapatanisha.

Kwa upande wake mwakilishi kutoka kituo cha ushauri na msaada wa kisheria mkoani hapa (PARALIGO) Avelina Mahundu “Kiukweli mkoa wa mtwara unaongoza kwa akina baba wanapoachana, kutengana au kuzaa tu na msichana hawaoni umuhimu wa kumchukua mtoto au kuhudumia mtoto kwahiyo anaacha mke na mtoto”,Amesema  

Mmoja wa washiriki hao Fatuma Jamungu kutoka kata ya Msimbati kuhusu mafunzo hayo amesema, tofauti na hapo awali hivi sasa kupitia mafunzo hayo mambo mengi ameyapata juu ya ukatili wa kijinsia na atakuwa sehemu ya uelimishaji wa elimu hiyo katika kata yake.

Comments

Popular posts from this blog

Wananchi wajenga wodi baada ya kuchoshwa na kujifungulia sakafuni

Sita wapotea katika mazingira tatanishi wilayani Wete

Jaji Mkuu Zanzibar awashukia mahakimu wanaonyanyasa watuhumiwa