Mamlaka ya Bandari Mtwara yaipiga tafu hospitali ya Rufaa Mtwara

Na, Florence Sanawa,
Sauti ya Mnyonge, Mtwara

MAMLAKA ya Bandari Tanzania Mkoa wa Mtwara  imewakumbuka wanyonge Hospitali ya Rufaa Ligula kwa kutoa shuka 100 zenye thamani ya zaidi ya shilingi 1,300,000 ambapo inapelekea Hospitali hiyo kuwa na upungufu wa shuka 800 tu kwa sasa.

Akipokea shuka hizo Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo Dickson Sahini alisema kuwa hospitali hiyo ina vitanda 248 ambapo vinatakiwa kuwa na shuka 8 kwa kila kitanda hali ambayo inakuwa ngumu kutokana na uhaba uliopo hospitlaini hapo.

hospitali hiyo ilikuwa na upungufu wa shuka 900 ambapo baada ya kupata hizo wanaupungufu wa shuka 800 ili kupata shuka 8 kwa kila kitanda kama taratibu zinavyotakiwa kuwa.

“Tunayo pia changamoto ya uboreshaji wa majengo ambayo hivi sasa ni chakavu, tuna tatizo kubwa la uhana wa  vifaa tiba, vifaa vishirikishi ikiwemo mashine ya kufulia” alisema Sahini

Kwa upande wake Mkuu wa Bandari Mkoa wa Mtwara Nelson Mlali alisema kuwa mamlaka hiyo imeamua kutoa shuka hizo ili kuweza kuisaidia jamii.

“Hatuwezi kutatua kila changamoto lakini tumenzia kwenye shuka mengine tutajitahidi kuwasiliana nao ili kuweza kutengneza mazingira mazuri kwa jamii yetu” alisema Mlali

Comments

Popular posts from this blog

Wananchi wajenga wodi baada ya kuchoshwa na kujifungulia sakafuni

Sita wapotea katika mazingira tatanishi wilayani Wete

Jaji Mkuu Zanzibar awashukia mahakimu wanaonyanyasa watuhumiwa