Mtuhumiwa wa kosa la ubakaji aachiwa huru

Na, Mwandishi Wetu,
Sauti ya Mnyonge, Zanzibar

BAADA ya kusota rumande kwa kipindi cha zaidi ya miezi miwili , hatimaye kijana Njile Masalu  Nchilu mkaazi wa Kifumbikai Wete , ameachiwa huru na mahakama ya mkoa wa Kaskazini Pemba.

Kijana huyo aliyekuwa anatuhumiwa kwa kosa la kubaka ameachiwa huru na mahakama hiyo baada ya shahidi namba moja ambaye ndiye mwathirika wa tukio hilo kukana kufanyiwa kitendo hicho .

Msichana huyo mwenye umri wa miaka 15 , amekana kufanyiwa kitendo hicho mbele ya hakimu wa mahakama hiyo Makame Mshamba Simgeni na mwendesha mashtaka wa serikali Ramadhan Suleiman Ramadhan , jambo ambalo limeifanya mahakama kuliondoa shauri hilo mahakamani hapo .

Baada ya mahakama kuliondoa shauri hilo , kijana Njile aliondoka nduki kali katika viwanja wa mahakama , mithili ya wakimbiaji wa mbio za relay , huku akiwa haamini kilichotokea.

Njile alikuwa anakabiliwa na tuhuma ya kumbaka msichana mwenye umri wa miaka 15 , kosa ambalo alidaiwa kwamba amelitekeleza septemba 5 mwaka 2017.

Comments

Popular posts from this blog

Wananchi wajenga wodi baada ya kuchoshwa na kujifungulia sakafuni

Sita wapotea katika mazingira tatanishi wilayani Wete

Jaji Mkuu Zanzibar awashukia mahakimu wanaonyanyasa watuhumiwa