Mbunge ahofia uhaba wa wataalamu sekta ya afya nchini
Na, Mwandishi Maalum Sauti ya Mnyonge, Dodoma MBUNGE wa Hanang Dk.Mery Nagu (CCM) ameonesha kuwa na wasiwasi kuwa kuna uwezekano wa viongozi kuhamasisha ujenzi wa vituo vya afya pamoja na zahanati lakini wasiwepo wataalamu wa sekta ya afya kutokana na kutokuwepo kwa watumishi wa kutosha. Akiuliza swali jana bungeni Dk.Nagu aliitaka Serikali ieleze ina mikakati gani ya kuongeza watumishi wa sekta ya afya katika vituo mbalimbali vya afya na zahanati kutokana na kukosekana kwa wataalam. “Je si kazi bure kama wananchi watajenga vituo vya Umma vya afya na zahanati lakini havitumiki je serikali ina mpango gani wa kuongeza watumishi katika vituo hivyo licha ya kuwepo kwa upungufu mkubwa wa watumishi katika sekta hiyo” alihoji Dk.Nagu. Awali katika swali la msingi la mbunge wa Busanda Lolensia Bukwimba (CCM) alitaka kujua serikali ina mkakati gani wa kuondoa uhaba wa watumishi wa sekta ya afya katika mkoa wa Geita kutokana na tatizo hilo kuwa kubwa. “Tatizo la uhaba wa watumishi katika sekta y...