Serikali kujenga kituo kikubwa kutibu "mateja" mjini Dodoma

Na, Mwandishi Maalum
Sauti ya Mnyonge, Dodoma

SERIKALI imepanga kuanzisha kituo kikubwa cha kuwapatia tiba waathirika wa dawa za kulevya kwa njia ya kazi kituo kitajengwa Mkoani Dodoma.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi Ajira naVijana,Antony Mavunde alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Kiembesamaki Ibrahim Mohamed  Raza (CCM) Katika swali lake Raza alitaka kujua  ni lini serikali itachukua hatua kwa kuwasaidia vijana walioathirika na matumizi ya dawa za kulevya .

Mavunde alisema serikali inatambua tatizo la matumizi ya dawa za kulevya na athari zake kwa vijana .

Alisema katika kukabiliana na hilo Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imekuwa ikichukua hatua kadhaa kuwasaidia vijana hao .

Alisema moja ya hatua ni pamoja na kutoa tiba kwa waathirika ambapo hadi kufikia mwishoni mwa mwaka jana jumla ya vituo vitano vya tiba ya methadone vilisha anzishwa.

Mavunde alisema vilianzishwa katika Hospitali ya Muhimbili, Temeke, Mwananyamala, Zanzibar na Mbeya.

Alisema kupitia vituo hivyo waraibu 5,830 walipatiwa tiba na wengine wanaendelea kupata tiba.

Katika kipindi cha mwaka huu serikali inatarajia kufungua vituo vipya vya tiba katika mikoa ya Mwanza na Dodoma.

Alisema kutokana na utafiti uliofanywa mwaka 2014,Serikali imepanga kufungua vituo vingine vya tiba katika mikoa ya Pwani, Morogoro, Arusha, Kilimanjaro na Tanga.

Alisema kazi hiyo itafanyika kulingana na upatikanaji wa fedha serikalini.

Comments

Popular posts from this blog

Wananchi wajenga wodi baada ya kuchoshwa na kujifungulia sakafuni

Sita wapotea katika mazingira tatanishi wilayani Wete

Jaji Mkuu Zanzibar awashukia mahakimu wanaonyanyasa watuhumiwa