Uendeshaji shule wakwama baada ya wajumbe wa bodi kususia vikao "visivyo na kitu"
Na, Florence Sanawa
Sauti ya Mnyonge, Mtwara
WAJUMBE wa bodi za shule mkoani Mtwara wamesusia kuhudhuria vikao vya uendeshaji wa shule kutokana na kutolipwa posho baada ya serikali kutangaza dhana ya elimu bila malipo.
Shirika la faidika wote kwa pamoja (FAWOPA) lilibaini hali hiyo wakati wa mradi wa ufuatiliaji wa matumizi ya rasirimali za umma katika sekta ya elimu manispaa ya mtwara mikindani kutoka kutembelea shule mbalimbali na kubaini kusimama kwa maamuzi mengi.
Akizungumza katika kikao cha wadau wa elimu kilichoandaliwa na shirika la faidika wote kwa pamoja (FAWOPA) ambapo maafisa watendaji kata, walimu wakuu, wachumi, wazazi na maafisa elimu walihudhuria, Mratibu wa shirika hilo Baltazar komba alisema kuwa vikao vingi vilisimama baada ya serikali kutoa agizo la elimu bure.
Alisema kuwa kukwama kutokana na kutokuwepo kwa michango shuleni hivyo wajumbe hao kukosa posho ya kujikimu hali ambayo inawafanya walimu wachukue maamuzi wenyewe.
“Hivi vikao vya bodi za shule visipo endelea maamuzi yatakuwa yanatolewa upande wa walimu tu hali ambayo inaweza kuchangia kudorola kwa elimu nchini na kusimama kwa maendeleo ya shule zetu tushirikiane kuzikumbusha mamlaka kuchukua hatua ili vikao hivi virudi na maamuzi yachukuliwe”alisema Komba
Nae Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Sabasaba Musa Mponda anasema kuwa hivi sasa hali sio nzuri kutokana na vikao bodi za shule havifanyiki.
“Kikifanyika kikao kimoja wajumbe 15 wanapaswa wadhurie ambapo wanalipwa shilingi 70,000 kwa kila mmoja changamoto inakuja shule hazina miradi na miradi iliyopo haiwezi kusaidia kuchatatua hilo hali inayopelekea vikao kusimama na pale maamuzi yanapohitajika hufanywa na walimu” alisema Mponda
Kwa upande wake Mkuu wa Shule ya Sekondari Rahaleo Julius Mkuwele anasema kuwa kukosekana na posho kunasimamisha maendeleo ya shule nyingi hali ambayo inazifanya shule hizo kukaa bila kuendelezwa kwa muda mrefu kutokana na watoa maamuzi kushindwa kukaa vikao.
“Mwaka jana shule moja iliita kikao cha bodi wa jumbe hawakufika hata mmoja kikao hakikufanyika kutokana na idadi haikutosha hii inawapa wakati mgumu wakuu washule pale wanapotaka kuitisha vikao unakuwa na maswali mengi kichwnai juu ya posho ya wajumbe la sivyo utajikuta unaita walimu mnafanya maamuzi wenyewe hii ni hatari kwa mustakabali wa maendeleo ya elimu mkoani kwetu” alisema Mkuwele
Comments
Post a Comment