Wataka minada ya korosho kusitishwa kufuatia bei kushuka

Na, Marry Sanyiwa
Sauti ya Mnyonge, Mtwara

Wakulima wa korosho wa wilaya ya Tandahimba na Newala Mkaoni Mtwara,wakifungua sanduku la tenda katika mnada wa kumi na mmoja ambao ulifanyika katika kijiji cha  kitama ya kwanza wilayani humo.

Wakulima wa zao la Korosho wa wilaya ya Tandahimba na Newala Mkoani Mtwara, wameishinikiza Bodi ya Korosho Tanzania (CBT) kusitisha kuendelea kwa minada ya korosho ghafi kutokana na bei ya zao hilo kuanza kushuka.

Akizungumza katika mnada wa Kumi na moja uliofanyika katika kijiji cha kitama ya kwanza wilayani tandahimba  Mkulima wa zao hilo Selemani Chiwinde  anasema kwa sasa wanunuzi wamepungua kwa kiasi kikubwa hivyo hawezi kuleta ushindani wa soko katika zao hilo wakati minada inaanza.

Alisema kuwa bei za minada imekuwa ikishuka siku hadi siku hadi kutoka bei juu ya shilingi 4128 hadi kufikia bei chini shilingi elfu 3400 hali ambayo inawatia hofu wakulima.

“tunaiomba Bodi ya korosho wafanye mnada huu kuwa wa mwisho kwa sababu yanayojitokeza kwa sasa  ya kushuka kwa bei katika minada hii ya mwisho ndio yale ambayo yalijitokeza katika msimu 2016/2017.” Anasema  Chiwinde

Naye Makamu mwenyekiti wa TANECU Shaibu Njauka anasema kuwa CBT wamekuwa wakishirikiana kwa mambo mbalimbali katika kufanikisha zoezi la biashara hii ya korosho katika mismu yote pindi  inapoanza.

“tunashirikiana vizuri na Bodi ya korosho ila wao wanaangalia sana sheria sisi kama wakulima tumekubaliana mnada huu uwe wa mwisho,hatukusudi kuvunja sheria ila tunalinda maslahi ya Mkulima kutokana na bei za korosho zimeanza kushuka tangu  mnada wa 10 hadi 11.” Anasema Njauka

Wakulima wa korosho wa kisikiliza bei ya minada baada ya kusomwa kwa bahasha ambazo zilitenda katika mnada huo

Kwa upande wake Meneja wa Chama Kikuu cha Ushirika Tanecu Mohamed Nassoro ametoa angalizo kwa viongozi wa vyama vya msingi wilayani humo ambao wanataka kutumia nafasi ya kushuka kwa minada kunyonya fedha wakulima.

“natoa angalizo kwa baadhi ya viongozi wa chama cha Msingi wanaotaka kutumia nafasi ya kushuka kwa bei za mauzo ya korosho ya mnada wa kumi (10) kuwalipa wakulima ambao korosho zao waliuza katika mnada wa tisa(9) jambo hili halikubaliki mkulima alipwe kwa kile ambacho anastahili kulipwa.” Alisisitiza Meneja huyo

Akizungumza na hali hiyo Mwakirishi wa Bodi ya Korosho Tanzania (CBT) Jemes Jason anasema kuwa sheria iliyopo inavitaka vyama vya ushirika kuuza  korosho kwa mnada  kupitia mfumo wa stakabaadhi ghalani hivyo  mwenye mamlaka ya kusitisha au kufunga minada ni Bodi ya korosho na sio mtu mwingine.

Pia Jason amewashauri wakulima wa zao hilo katika wilaya ya Tandahimba na Newala kuendelea na minada hadi pale korosho zitakapokuwa zimekwisha katika maeneo yao ili waendelea kuuza zao hilo

Comments

Popular posts from this blog

Wananchi wajenga wodi baada ya kuchoshwa na kujifungulia sakafuni

Sita wapotea katika mazingira tatanishi wilayani Wete

Jaji Mkuu Zanzibar awashukia mahakimu wanaonyanyasa watuhumiwa