TRA yakusanya bilioni 16.7 katika majengo

Na, Mwandishi Maalum
Sauti ya Mnyonge, Dodoma

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imekusanya jumla ya sh. Bilioni 16.7 ikiwa ni kaodi ya majengo mbalimbali.

Kauli hiyo ilitolewa jana bungeni na Naibu Waziri wa Fedha Dk. Ashatu Kijaji alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Kavuu  Dk.Prudenciana Kikwembe (CCM)

Dk.Ashatu alisema kwa mujibu wa Sheria ya fedha ya mwaka 2017 kifungu cha 64 kimebainisha kuwa TRA itakusanya kodi za majengo.

Alisema ukusanyaji huo utafanyika katika Majiji, Miji na Miji midogo yote nchini badala ya Mamlaka za serikali za Mitaa.

Naibu Waziri alisema kwa kuwa majengo mengi hayajafanyiwa uthamini Serikali kupitia Bunge lilifanya uamuzi wa kuweka kiwango maalum cha kulipa.

Alisema kiwango hicho ni Sh.10,000 kwa majengo ya kawaida n ash. 50,000 kwa majengo ya ghorofa.

“Viwango hivi ni vya mpito wakati serikali inakamilisha zoezi la uthamini kwa majengo yote yanayostahili kulipiwa kodi ya majengo.

Alisema majengo yote yaliyofanyiwa uthamini yanalipiwa viwango stahiki kulingana na uthamini.

Katika swali lake Dk.Prudenciana alitaka kujua ni kwanini Manispaa mbalimbali zinatoza kodi zaidi ya zile zilizopangwa na Bunge.

Comments

Popular posts from this blog

Wananchi wajenga wodi baada ya kuchoshwa na kujifungulia sakafuni

Sita wapotea katika mazingira tatanishi wilayani Wete

Jaji Mkuu Zanzibar awashukia mahakimu wanaonyanyasa watuhumiwa