SERIKALI: hata sarafu za zamani bado ni halali na zinatumika

Na, Mwandishi Maalum
Sauti ya Mnyonge, Dodoma

IMEELEZWA kuwa  sarafu zote zilizowahi kutolewa na Benki Kuu Tanzania(BOT) tangu mwaka 1966 bado ni halali kwa matumizi nchini na zinatumika kwenye miamala ambayo si ya fedha taslimu.

Kauli hiyo ilitolewa bungeni jana na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dk.Ashatu Kijaji alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Kuteuliwa Salma Kikwete (CCM).

Mama Salama Katika swali lake alisema vijana waliozaliwa  kuanzia miaka ya 1990 na kuendelea hawazijui sarafu za senti 5, 10, 20, 50,.

 “Kwanini serikali haioni ni wakati muafaka sasa kurudisha sarafu hizo kwenye mzunguko ili vijana wengi waweze kuzijua” alisema..

Dk.Ashantu alisema alisema BoT imepewa kisheria jukumu la kuzalisha fedha za noti na sarafu kulingana na mahitaji na mazingira ya kiuchumi yaliyopo.

Alitaja mambo muhimu yanayozingatiwa wakati wa kuondoa na kuingiza katika soko noti na sarafu ya thamani ndogo na kubwa ni mfumuko wa bei wa bidhaa za huduma, kulinda thamani ya shilingi na wepesi wa sarafu kubebeka.

Alisema  sarafu za shilingi zenye thamani ndogo ikiwemo senti 5,10, 20, 50 pamoja na shilingi 1,5,10 na 20 kwa uhalisia ubebaji wake ni mgumu.

Naibu Waziri pia alisema nchi haina sera ya kupanga bei ya bidhaa na huduma kwasasa, ni vigumu kurejesha sarafu hizi katika mzunguko wa fedha.

Akizungumzia  mada ya shilingi na senti kufundishwa mashuleni, Dk.Kijaji alisema maarifa ya mada hiyo yanatolewa shuleni ili kuwapa wanafunzi maarifa ya kihesabu na pia zinaweza kuombwa kwa ajili ya kuwafundishia.

Comments

Popular posts from this blog

Wananchi wajenga wodi baada ya kuchoshwa na kujifungulia sakafuni

Sita wapotea katika mazingira tatanishi wilayani Wete

Jaji Mkuu Zanzibar awashukia mahakimu wanaonyanyasa watuhumiwa