Wamiliki bodaboda watakiwa kuwapa mikataba wanaowaajiri kuziendesha, na kutakiwa kuzikatia bima kubwa

Na, Mwandishi Maalum
Sauti ya Mnyonge, Dodoma

WAAJIRI nchini wanaotoa ajira kwa vijana waendesha pikipiki au bajaji wametakiwa  kuzingatia sheria ikiwa ni pamoja na kuwa na mikataba.

Hayo yalisemwa jana bungeni na  Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi Ajira na Vijana Anthony Mavunde alipokuwa akijibu swali.

Mavunde alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Uzini  Salum Mwinyi Rehani (CCM) aliyetaka kujua ni lini serikali itawatambua rasmi dereva wa bodaboda  au bajaji kwa kuwaandikia mikataba na kuwawekea akiba  na kulipiwa mifuko ya Hifadhi ya jamiii.

Mavunde alisema kuwa mbali na mikataba pia waajiri hao wanatakiwa kuhakiokisha waajioriwa wao wanapata huduma zingine muhimu zinazowawezesha kufanya shughuli zao kwa ufanizi na kwa kuzingatia usalama wa uhai wao na vyombo vyao.

Alisema serikali itaendelea kusimamia matakwa ya sheria yanayomtaka mwajiri kutoa mikataba hiyo ikizingatiwa kwamba mkataba unabeba haki za msingi na wajibu kwa kila upande.

“Nichukue fursa hii kutoa maagizo kwa waajiri wote kuhakikisha kuwa madereva wao wa bodaboda na bajaji wanakuwa na mikataba” alisema

Aidha alisema serikali ilisha watambua rasmi madereva hao wa bodaboda na bajaji toka mwaka 2009.

Naibu Waziri alisema ili madereva hao waweze kutambuliwa kwa urahisi kwa lengo la kupatiwa huduma mbalimbali zikiwemo za hifadhi za jamii, serikali imefanya juhudi kubwa la kuwashawishi kujiunga katika vikundi.

Alisema kupitia vikundi hivyo Elimu juu ya masuala ya Sheria za kazi na Hifadhi ya jamii hutolewa.

Wakati huo huo, mbunge wa Babati Mjini,Pauline Gekul (Chadema) ameihoji serikali ni kwanini isione umuhimu wa kuwalazimisha wamiliki wa Bajaji na Bodaboda kukata bima kubwa kwa vyombo hivyo vya usafiri ili kuweza kumlinda mwendeshaji wa vyombo hivyo pale anapopata ajali.

Gekuli aliuliza swali la nyongeza jana ambapo alitaka  kujua ni kwanini serikali isiweze kukaa na wamiliki wa Bodaboda au bajaji ili waweze kuzikatia bima kubwa ili kulindaa maisha ya mwendeshaji wa vyombo hivyo pale inapotokea ajali na mwendeshaji wa chombo hicho kuumia.

“Kwa kuwa vijana wengi ambao wanaendesha vyombo vya usafiri kama vile bajaji na bodaboda wanapata ajali wanapokuwa katika shughuli zao za kila siku na wanaumia.

"Lakini wamiliki wa vyombo hivyo hawakati bima kubwa je ni ni kwani serikali isione umuhimu wa kukaa na wamiliki wa vyombo hivyo wakakata bima kubwa ili pale madereva wanapopata ajali iwe nafuu kwa kupata huduma ya fidia na matubabu” alihoji Gekul.

Akijibu maswali hayo Naibu Waziri,Kazi,Vijana na Ajira –TAMISEMI Anthony Mavunde alisema suala la wamiliki kukata bima kubwa kwa ajili ya vyombo vya moto kama vile bajaji na pikipiki serikali itaangalia uwezekano wa kukaa na wamiliki ili kuweza kufanya hivyo.

Aidha alisema njia pekee na raisi kwa vijana ambao ni madereva pikipiki na Bajaji ni kujiunga katika vikundi mbalimbali kwa lengo la kuweza kujuinga katika mifuko mbalimbali ya jamii.

Comments

Popular posts from this blog

Wananchi wajenga wodi baada ya kuchoshwa na kujifungulia sakafuni

Sita wapotea katika mazingira tatanishi wilayani Wete

Jaji Mkuu Zanzibar awashukia mahakimu wanaonyanyasa watuhumiwa