Wananchi Nyakatanga wasema sasa wana uhakika wa maisha

Na, Mack Ngaiza
Sauti ya Mnyonge, Kanda ya Ziwa

Wananchi wa kata ya Nyakatanga wilayani Muleba, wamesema kuwa uhakika wa maisha yao yameanza kupata ufumbuzi kutokana na kujengewa zahanati baada ya kuishi kwa shida wakitembea zaidi ya kilomita10 kufuata huduma ya afya.

Wametoa kauli hiyo na kuiomba serikali kuharakisha kutuma wauguzi kwenye zahanati hiyo, baada ya kutembelea ujenzi wa zahanati hiyo.

Mkuu wa Mkoa wa Kagera,Mhe. Meja Jenerali MST Salum M. Kijuu leo tarehe 30/01/2018 ametembelea na kukagua shghuli za Ujenzi wa zahanati ya Nyakatanga iliyojengwa kwa ufadhili wa shirika la World Vision,mchango wa Mbunge Jimbo la Muleba Kaskazini Mhe. Charles Mwijage (Waziri wa Viwanda, Uwekezaji na Biashara) na nguvu ya jamii.

Mradi huu umegharimu kiasi cha Tsh. 56,761,100 kati ya hizo, World Vision imechangia kiasi cha Tsh 47,000,000.00 Mbunge wa jimbo la Muleba Kaskazini, Mhe. Charles Mwijage amechangia Tsh. 5,451,000.00 na wananchi wamechangia kiasi cha Tsh. 4,310,000. 

Uongozi wa kata unaendeleaje kuhamasisha wananchi kuchangia ili kukamilisha ujenzi wa kichomea taka na Nyumba ya Mtumishi.          
                         
Awali kata nzima haikuwa na zahanati na wananchi walitibiwa katika zahanati ya kata jirani kata Mushabago.                      

Wananchi wametoa shukrani kwa Shirika la World Vision na Mbunge kwa kufadhili mradi huo.

Comments

Popular posts from this blog

Wananchi wajenga wodi baada ya kuchoshwa na kujifungulia sakafuni

Sita wapotea katika mazingira tatanishi wilayani Wete

Jaji Mkuu Zanzibar awashukia mahakimu wanaonyanyasa watuhumiwa