Vyoo vipya vyavutia wanafunzi kuhudhuria masomo
Na Florence Sanawa
Sauti ya Myonge, Mtwara
UJENZI wa vyoo vipya katika Shule ya Msingi Madimba umeongeza hamasa kwa wanafunzi wa shule hiyo kuhudhuria masomo darasani hivyo kupunguza tatizo la utoro shuleni hapo.
Akizungumza wakati akipokea matundu 8 ya vyoo kutoka TPDC Mwalimu Mkuu Shule ya Msingi Madimba Hamis Nambunga utoro huo ulitokana na uhaba wa vyoo uliokuwepo shuleni hapo.
Alisema kuwa watoto wengi hasa wenye matatizo mbalimbali walishindwa kuhudhuria masomo na kufanya utoro uwe mkubwa kwakuwa walikosa mahali pa kujihifadhi kutokana na vyoo vya shule hiyo kutokuwa na mazingira ya kuridhisha.
Nambunga alisema kuwa baada ya shirika hilo kuwajengea matundu 8 sawa na asilimia 48 pekee wanaomba serikali na wadau wengine waweze kujitokeza ili kuweza kuboresha mazingira vyoo shuleni hapo ambapo hivi sasa matundu 10 ndio yanahitajika.
“Hali ilikuwa mbaya ilifkikia wakati serikali ilitaka kufunga shule yetu kutokana na tatizo la choo ujenzi wa hule hii utaongeza hamasa ya wazazi na serikali kutupa msaada wa vyoo vingine ili kuendeleea kutunza na kulinda mazingira ya vyoo vyetu.
Akikabidhi vyoo hivyo kwa mkuu wa shule Meneja mradi wa kiwanda cha kusafisha na kuchakata gesi Madimba ambaye pia ni Mwakilishi wa Shirika la Petrol Tanzania (TPDC) Sultan Pwaga alisema shirika letu liliahidi kuboresha mazinginra ya vyoo baada ya kupata taarifa ya uhaba wa vyoo shuleni hapo.
Alisema kuwa shirika hilo litaendelea kushirikiana ili kuboresha mazingira ya wanafunzi katika shule hiyo sambamba na kuwaboreshea huduma ya maji kwa kushirikiana na serikali ya kijiji.
“Wazazi walimu na wanafunzi tunaimani watashirikiana kutunza miundombinu hii kwa faida ya jamii nzima ya madimba ikiwemo kukamilisha suala la maji ambalo ndio litasaidia kutunza miundombinu ya vyoo hivyo….
“Tumekuwa na ushirikiano kwa muda sasa na kijiji hichi ndio maana tunajithidi kuisaidaia jamii inayotuzunguka ili kuweza kuiweka katika marinzignra bora safi na salama” alisema Pwaga
Comments
Post a Comment