Soma kilio cha maumivu ya kisaikolojia anacholia mama huyu aliyebakwa

Na, Shirazy Haroub
Sauti ya Mnyonge, Pemba

MWANANMKE mmoja (30) mkaazi wa Kiungoni  Wete Pemba, anaendelea kuteseka kiakili  na kimwili,  baada ya kudai kuwa amebakwa na kunajisiwa na kijana aliemtaja kwa jina la Mohamed Omar Khamis, ambae ni  mtoto wa sheha wa shehia ya Kiungoni wilayani humo.

Picha ya Mtandaoni, ikimuonyesha mwanamke
anayedondokwa na chozi
Akizungumza kwa huzuni  huko nyumbani kwao Kiungoni mwanamke huyo alisema,  tukio hilo lilitokea kipindi cha nyuma, ambapo alikutwa na mkasa huo, alipokwenda porini kutafuta kuni, ndipo ghafla alimuona kinana huyo na kuanza kumfuata nyuma huku akiwambia kuwa anataka kufanyanae mapenzi.

“Alikua ananiuliza, kwa sauti ya chini juu ya kutaka kufanya mapenzi na mimi ingawa nilikuwa nakataa na kuanza kumkimbi kimbia, lakini  mwisho akanivamia ghafla na kisha na kuniangusha chini'', alisema mweanamke huyo. 

Alifafanua kuwa, baada ya kufanyiwa tukio hilo alikurupuka na kwenda  mbio, ingawa kumbe kulikua na mwenzake aliyemtaja kuwa ni Mohamed Khamis Hamad  nae alitaka pia alitishi kumbaka.

'' Wakati naondoka nilimuona huyu mtoto wa sheha ananicheka kumbe kulikua na rafiki yake na alikuwa na mbwa, walikua pamoja akanambia nisogee na nikijaribu kukimbia atanifukuzisha mbwa , lakini sikuogopa nikafanikiwa kukimbia'' ,alisema mwanamke huyo.

Alisema, kinachomsikitisha zaidi , ni kutakiwa kuwaomba msamaha familia ya mtuhumiwa kwasababu amefanyakosa kuliripoti tukio hilo kituo cha polisi.

''Wanasema, mimi nimekosea sana, nikawaombe radhi , kwanini  sijawaambia tukakaa pamoja tukalimaliza, eti nimefanya haraka kulipeleka polisi,'' alisema mwanamke huyo.

Akizungumza na waandishi wa habari kaka wa mwanamke huyo ambae pia jina lake tunalihifadhi alisema, tukio hilo limewasikitisha sana na linaendelea kuwatesa.

Alisema, mara baada ya ndugu yake kumpa taarifa hizo ,walikwenda kuripoti kituo cha Polisi Mchangamdogo na hatua zinaendelea ingawa alisema inaonekana kuna jitihada za makusudi za kuliuwa tukio hilo, ili lisiendelee tena.

''Baba mzazi wa mtuhumiwa (ambae ndie sheha wa shehia ya Kiungoni) analeta vitisho , eti anasema tukiendelea kushikilia atatufunga, lakini sisi tunasema tukio lishafika Polisi,'' alisema kaka huyo.

Kaka huyo, aliendelea kueleza kuwa, katika mchakato wa kutaka kulimaliza tukio hilo kienyeji, familia ya mtuhumiwa imekua ikiwafuata mara kwa mara, ili walimalize wenyewe pasi na kushikilia kulipeleka katika ngazi za kisheria husika.

Kwa upande wake sheha wa shehia ya Kiungoni, Omar Khamis Othman ambe ndio baba mzazi wa mtuhumiwa, alipofuatwa na waandishi wa habari hizi alisema kuwa, tukio hilo lipo na analifahamu, ingawa halijaripotiwa rasmi katika afisi yake.

Kamanda wa Polisi mkoa wa kaskazini Pemba Haji Khamis Haji alikiri kutoke kwa tukio hilo tokea Januari 3 mwaka huu, na liliripotiwa kituo cha Polisi Mchangamdogo Januari 10, mwaka 2018.

Aliwataja watuhumiwa wa tukio ambao ni wale wale aliyowataja mdai kuwa ni Mohamed Omar Khamis (17) anaesemwa kuwa ni mtoto wa sheha) na Mohamed Khamis Hamad  (19).

Kamanda alisema tukio lililoripotiwa ni shambulio la aibu na wanaendelea kufanya mahijiano juu ya tukio hilo na ikibainika kuna ubakaji watabadilisha hati ya mashtaka na kuweka kosa la ubakaji .

Comments

Popular posts from this blog

Wananchi wajenga wodi baada ya kuchoshwa na kujifungulia sakafuni

Sita wapotea katika mazingira tatanishi wilayani Wete

Jaji Mkuu Zanzibar awashukia mahakimu wanaonyanyasa watuhumiwa