Mkuu wa Mkoa atoa miezi mitatu wananchi kujisajili daftari la wakazi
Na, Florence Sanawa
Sauti ya Mnyonge, Mtwara
MKUU wa Mkoa wa Mtwara Gellasius Byakanwa ameagiza ndani ya miezi mitatu kwa wananchi wa mkoa huo kujiandikisha katika daftari la makazi.
Akizindua daftari hilo jana alisema kuwa ili kuimalisha ulinzi na usalama wa mkoa wanannchi wanapaswa kujiandikisha katika kipindi hicho bila kukosa.
Alisema kuwa andikishwaji wa daftari hilo utasaidia kutatua masuala ya kiharifu yanayotokea katika mitaa yetu hivyo wananchi wanapaswa kufahamiana ili kudumisha amani ya mkoa.
“Hili zoezi hilo sio la kupoteza muda kutokana na umuhimu wa usalama na maendeleo ya nchi, ili serikali iweze kutusaidia lazima ijue idadi yetu hapo ndio bajeti inaweza kupangwa kulingana na idadi ya watu na mahitaji yaliyopo ndani ya jamii hatutaweza kuondoka katika umasikini bila kujua idadi yetu……
“Daftari hili limeandaliwa tangu 2011 halijawahi kutumika hata wakuu wa mikoa waliotangulia hakuwahi kujiandikisha wala kujua mwenyekiti wao wa mtaa ninani ndio maana nitoa miezi mitatu kwa wakazi wote wa mkoa huu kujiandikisha katika daftari hilo bila kukosa”
“Tusipofahamiana tunaweza kulea uharifu kwa kiasi kikubwa ili tuondokane na yali ya sintofahamu na kuendelea kulinda amani yetu sehemu kubwa tunaweza kuifanya kama tukifahamiana na pia ipo sehemu ya kutambua wafanyabiashara hii itatusaidia hata kwenye masuala ya makusanyo ya mapato”
“Hakuna mtu atakaetaka barua yoyote ama kitambulisho chochote kama sambamba na zile za kufungua akaunti, kuchukua mkopo ama kutaka barua yoyote bila kujiandikisha bila kuwepo kwenye daftari la makazi”
“Watendaji nisikilizeni vizuri mmezoea tu mtu anakuja anataka barua ya utambulisho unaandika unapiga muhuri unampatia sasa nikikuta mtu kapewa barua bila kuwepo kwenye daftari nitachukua hatua”
“Wapo watu wanamigogoro ya kifamilia wakija hawajajiandisha msiwasuluhishe hadi wawe wamejiandikisha ikiwemo barua za utambulisho hautaipata kama haujajiandikisha”
“Tunapoandikisha lazima tuangalie mkuu wa kaya watu wote anaishi nao ndani ya nyumba na kujua wangapi wamesoma wangapi wana umri mkubwa lakini hawakupata elimu ya msingi ni vema tuwajue”
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara Mikindani Beatrice Dominic alisema kuwa kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya 2012 manispaa ya mtwara mikindani ina jumla ya watu (Laki moja na nane) huku kukiwa na ongezeko la watu kwa mwaka ni asilimia 1.6.
Alisema kuwa hadi sasa manispaa hiyo inadiliwa kuwa na wakazi (laki moja kumi na tano mia moja kumi na nne) wanaopaswa kujiandikisha hadi sasa wapo wakazi (arobaini na sita laki saba na nne) ndio waliosajiliwa hali ambayo inaonyesha kuwa na idadi kubwa ya wananchi ambao hawajajiandikisha.
“Unajua uandikishwaji huu katika daftari la makazi ni agizo la serikali ambalo linazitaka mamlaka za serikali za mitaa kuhakikisha kuwa wakazi wote katika mitaa wanaandikishwa katika daftari hilo………
Zoezi hilo lilikuwa linakwama kwakuwa wananchi walikuwa hawana uelewa juu umuhimu wa kujiandikisha katika daftari hilo ambalo tunapojiandikisha mamlaka zinaweza kujua hitaji la shule, zahanati na kuhifadhi takwimu za mtaa ili kusaidia kupanga mipango mbalimbali ya maendeleo” alisema Dominic
Comments
Post a Comment