Posts

Showing posts from March, 2018

Mbunge atoa msaada kituo cha watoto yatima cha Light in Africa

Image
Mmiliki wa kituo cha watoto yatima na wenye uhitaji maalum, cha Light in Africa cha Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro, Lynn Elliott akimpa mkono mbunge wa viti maalum wa Mkoa wa Manyara, Ester Mahawe, baada ya kupokea msaada wa vyakula na vifaa vya shule.  Mbunge wa viti maalum wa Mkoa wa Manyara,  Ester Mahawe (kulia) akimpa mkono wa pongezi mtumishi wa huduma ya Upendo wa Yesu ya Njiro jijini Arusha, Rachel Mmasi aliyetoa sh500,000 za msaada wa watoto yatima wa kituo cha Light in Africa cha Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro. Picha na Joseph Lyimo, Sauti ya Mnyonge, Manyara

Ahadi za JPM ujenzi wa barabara Manyara, zaanza kutekelezwa

Image
Na Joseph Lyimo Sauti ya Mnyonge, Manyara Ahadi za ujenzi wa barabara zilizotolewa na Rais John Magufuli wakati wa kampeni ya kugombea urais mwaka 2015 alipotembelea Mkoani Manyara, zipo kwenye mchakato wa utekelezaji wake.  Pia, utekelezaji wa miradi ya barabara za mkoa huo zilizopo kwenye ilani ya uchaguzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa mwaka 2015/2020 unafanyiwa kazi.  Meneja wa wakala wa barabara nchini Tanroads mkoani Manyara, mhandisi Bashiri Rwesingisa aliyasema hayo kwenye kikao cha bodi ya barabara ya mkoa huo, kilichofanyika juzi mjini Babati.  Mhandisi Rwesingisa alisema barabara ya Arusha-Kibaya-Kongwa, yenye urefu wa kilometa 336.6 inayopitia Losinyai wilayani Simanjiro na Dosidosi wilayani Kiteto, inafanyiwa upembuzi na usanifu wa kina.  Alisema kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina inaendelea kutekelezwa na mhandisi mshauri M/S Cheil Engeneering co Ltd ya Korea kaskazini na M/S Inter-consult Ltd ya Tanzania.  Alisema barabara ya Karatu-Mbulu-Haydom-Singida ya ur

Wananchi wajenga wodi baada ya kuchoshwa na kujifungulia sakafuni

Image
Na Florence Sanawa Sauti ya Mnyonge, Mtwara WANANCHI wa Kata ya Mnyeu yenye vijiji vine Wilayani Newala Mkoani Mtwara wamejitosa kujenga wodi na chumba cha kujifugnuliwa baada ya kuchoshwa na udongo wa vyumba hivyo hali ambayo inapelekea wanawake wengi kujifungulia sakafuni. Ujenzi huo ambao awali ulichangiwa na wakazi wa patao 3455 kwa kutoa shilingi 2000  na baadae kuongezeka kwa kutoa 10000 kwa kila kaya umeleta matuini hali ambayo imemfanya mkuu wa wilaya hiyo Aziza Mangasongo kuchangia mifuko 30 ya saruji ili kukamilisha jengo hilo ambapo mpaka sasa wametumia zaidi ya shilingi milioni 7. Akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani iliyoadhimishwa kijijini hapo Hawa Akram mkazi wa kijiji hicho alisema kuwa awali walikuwa wa kijifungulia kwenye chumba kidogo chenye vitanda viwili hali ambayo ili kuwa ikiwa weka kwenye hatari zaidi kutokana na wengine kujifungulia chini. Alisema kuwa kutokana tatizo hilo wanawake wengi wamekuwa wakidharirika hasa wanapotakiwa kujifu

Mkuu wa Wilaya aumia wanafunzi wa kike kukatisha masomo

Image
Na, Florence Sanawa Sauti ya Mnyonge, Tandahimba   MKUU wa Wilaya ya Tandahimba Mkoani Mtwara Sebastian Waryuba amesema kuwa wilaya hiyo inakabiliwa na tatizo kubwa la wanafunzi wakike kuacha shule wakiwa sekondari kutokana na kupata ujauzito wakiwa na umri mdogo. Akizungumza wakati wa kampeni ya kupiga vita mimba kwa watoto wakike mashuleni juzi alisema kuwa changamoto hiyo inapelekea kushuka kiwango cha elimu wilayani humo huku watoto wengi wakike wakiwa katika hatari zaidi kutoana na mimba za utotoni. Alisema kuwa shule za sekondari zinaongoza kwa wanafunzi kuacha shule hali ambayo ambayo serikali imezindua kampeni ikiwa ni mkakati ili kuweza kukomesha tatizo hilo ambalo limekuwa likikatisha ndoto za wanafunzi wengi wilayani humo. “Kwa sehemu kubwa kumekuwa na tabia ya wazazi kukaa na kukubaliana wakati wa ujauzito wa mtoto hali ambayo inawafanya wawe na sababu nyingi kuliko maelezo jambo ambalo linapelekea wialya kurudi nyuma kielimu…….. “Ili tuweze kufikia uchumi wa kati na kuifan

Waandishi wakana kuwa chanzo cha machafuko nchini

Image
Na Haji Nassor Sauti ya Mnyonge, Zanzibar WAANDISHI wa habari nchini, wamesema wao sio chanzo cha migogoro na machafuko yanayojitokeza, kabla au baada ya kumalizika chaguzi, bali ni baadhi ya wanasiasa kushindwa kuwa na uvumilivu kisiasa. Walisema kwa vile wapo baadhi wamekuwa ndio wamiliki wa vyombo vya habari, ndio wanaovitumia vibaya vyombo vya hivyi vya habari, na kueleza wapendavyo hata kama maelezo hayo, yanaashiria uvunjifu wa amani. Wakizungumza kwenye mkutano wa siku mbili wa kuangalia masuala ya utawala bora, uchaguzi na demokrasia kwa nchi za Afrika, uliofanyika Kunduchi beach hotel jijini Dar-es Salaam, ulioandaliwa na shirika la Actionaid walisema wao wanafanyakazi zao kwa kufuata misingi na sheria. Walisema wanasiasa, ambao baadhi wanamiliki vyombo vya habari wamekuwa wakisababisha machafuko na kisha mzigo huo kuelemezwa wanahabari, jambo ambalo sio sahihi. Mwandishi wa habari Ghania Jumbe kutoka TBC, alisema hakuna mwandishi hata mmoja, anaependa kujitokeza kwa machafuko

Wakulima wataka ripoti ya soko la kimataifa wakapambane nalo huko huko

Image
Na, Zuhura Juma Sauti ya Mnyonge, Pemba WAKULIMA wa mwani shehia ya Kiungoni Wilaya ya Wete Pemba, wameiomba Serikali kufanya utafiti wa kina juu ya Soko la kuuzia mwani Kimataifa, ili wajue jimsi ya kupambana nalo na kuweza kujipatia kipato cha kuridhisha kitakachowasaidia kuwakwamua na umaskini. Walisema   wamekuwa wakilima kilimo hicho kwa muda mrefu sasa, ingawa bado Soko limekuwa ni kikwazo kikubwa kwao, kutokana na bei ndogo wanayouzia, ambayo huzorotesha shughuli zao za kilimo cha Mwani.  Walieleza   iwapo Serikali itafanya utafiti wa kina kuhusu soko la kuuzia mwani Kimataifa na kujua kitu kinacholifanya soko hilo kuwa la kiwango cha  chini, ili kusaidia wakulima hao kujua kiwango kinachohitajika na kuweza kupambana na soko hilo na kujipatia kipato cha kuridhisha.  “Tunataka tujue je ni kweli mwani una bei ndogo kimataifa au ni wanunuaji wa hapa kwetu tu wanatukomoa?, hivyo Serikali itakapofanya utafiti tutajua sababu ya bei kuwa ndogo”, walisema wakulima hao. Mmoja wa wakulima

Wanawake Pemba waaswa kuhusu matumizi sahihi ya simu

Na Hanifa Salim Sauti ya Mnyonge, Pemba WANAWAKE wametakiwa kuhakikisha wanatumia simu kwa kufuata sheria sambamba na kujua haki na wajibu huku wakijua sehemu sahihi za kulalamika pindi tatizo la mtandao linapojitokeza. Wito huo umetolewa na Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA Zanzibar Esuwatie Aisa Masinga, wakati alipokua akizungumza na wanawake wajasiriamali katika semina ya siku moja iliyofanyika katika ukumbi wa Maktaba kuu Mjini chake chake Pemba.   Alisema kuwa, ipo haja ya kutoa elimu kwa wanawake ili kujua sheria za mitandao pamoja na kujua maana ya mamlaka ya mawasiliano Tanzania kwani wanawake wamekua wakifanyiwa makosa mengi katika mitandao ya kijamii. Alieleza kuwa, pamoja na udhalilishaji wa wanawake unaofanywa katika mitandao lakini bado jamii imekua ikishindwa kujua sehemu sahihi za kuripoti makosa hayo. “ Lengo ni kuwapa uelewa wanawake kuhusiana na mtandao wanapopata tatizo hasa katika mitandao ya kijamii hushindwa sehemu sahihi ya kulalamika kinachotakiwa

Walimu wa Madrasa Pemba wahimizwa kusaidia jamii

Image
Na, Zuhura Juma Sauti ya Mnyonge, Pemba WALIMU wa madrasa Kisiwani Pemba, wametakiwa kufanya kazi ya kuisaidia jamii katika kuendeleza Uislamu, sambamba na kuwa na Ikhlas, ili kuepusha changamoto zinazoweza kujitokeza. Akizungumza na walimu hao, Ofisa Fatwa na utafiti wa mambo ya Kiislamu kutoka Ofisi ya Mufti Kisiwani Pemba, Said Ahmad Mohamed ,katika mkutano wa kuelimisha walimu wa madrasa kuhusu vitendo vya udhalilishaji vinavyofanyika katika jamii, uliofanyika katika shehia ya Kiungoni Wilaya ya Wete, alisema hawatofikia lengo iwapo walimu hao hawatokuwa na Ikhlas. Alisema   walimu wa madrasa ni kigezo cha kufikisha ujumbe kwa jamii na ndie anaefundisha Uislamu, hivyo waogope ubaya wa vitendo vya udhalilishaji duniani na akhera na waisaidie jamii katika kuamrishana mema, ili kuepusha madhara na athari ya vitendo hivyo. “Mwalimu aepuke riyah, awe anamkusudia Allah  anapofanya shughuli zake, pia Ikhlas ithubutu, ili kuepuka changamoto zote”, alisema Ofisa huyo. Kwa upande wake, Mjumb

Maofisa Utumishi Pemba watakiwa kuhakiki vyeti vya wafanyakazi

Image
Na, Maryam Talib Sauti ya Mnyonge, Pemba Maofisa Utumishi wa Wizara na taasisi mbali mbali za Serikali Kisiwani Pemba, wametakiwa kutofumbia macho watendaji wao  wanaorudi masomoni na kuleta vyeti visivyo sahihi kwa ajili ya kufanyiwa marekebisho ya mishahara ili kuondosha kuitia hasara Serikali. Hayo yalielezwa na Ofisa Mdhamini, Ofisi ya Rais Katiba, Sheria Utumishi wa Umma na Utawala Bora Pemba, Masoud Ali Mohammed ,alipokuwa akibadilishana mawazo na Maofisa Utumishi hao  katika ukumbi wa Katiba na Sheria Pemba. Massoud, aliwaeleza  Maofisa Utumishi hao kuondokana na muhali na kujiridhisha na vyeti vinavyoletwa na watumishi wanaotoka masomoni katika kuwapatia stahiki zao ili kuepusha msongamano wa kuangamizana na kutiana katika matatizo yasiokuwa ya lazima. “Ndugu zangu maofisa utumishi nawaambieni ni wakati sasa wa kujitathmini tulikotoka na tonakokwenda tuangalieni wenzetu waliopita yaliowakuta tusifikire kwamba sisi tumefika hakuna atakaefumbia macho uovu tujihadhari na mapema ya

Wizara yasikia kilio cha madereva kuhusu alama tata ya barabarani

Image
Na Haji Nassor Sauti ya Mnyonge, Pemba BAADA ya malalamiko ya madereva kutoifahamu alama ya barabarani, iliopo eneo la Chamanangwe wilaya ya Wete Mkoa wa kaskazini Pemba, na kusababisha askari wa usalama barabarani kuwakamata, wizara ya Ujenzi, Miundombinu na Mawasiliano, imesema itaibadili alama hiyo. Akizungumza na mwandishi wa habari, hizi Mhandisi ujenzi wa kutoka wizara hiyo, Pemba Khamis Massoud, alisema inawezekana hao askari wanawakamata madereva kwa kutoifahamu matumizi yake. Alisema eneo hilo lenye usawa mrefu, na kutanguliwa na alama ya kumruhusu dereva aende mwendo atakao, lakini wapo baadhi ya askari huwakamata madereva pale wanapopindukia alama 40. Alisema inawezekana kweli, wapo baadhi ya madereva wamekuwa hawazielewi alama hizo, na wengine kwenda mwendo wa pole au wa kuibia hadi wa alama 60 ay 70 na wanapokamatwa hushindwa kujitetea. “Ni kweli unaweza kupishana na dereva anaendesha mwendo wa alama 40 katika eneo hilo,  kama kule aliokotokea kwenye mipindo na mikusanyiko

Utukufu wa viongozi wa dini unavyotiwa dosari na wachache wao

Image
Na Zuhura Juma Sauti ya Mnyonge, Pemba VIONGOZI wa dini ni watu watukufu katika jamii, ambao husikilizwa na waumini wao kwa kila wanachokisema na hufuatwa kwa kila wanachokiongoza. Miaka ya hivi karibuni, hali hiyo imekuwa ni tofauti kutokana na wachache wao kujihusisha na vitendo vya udhalilishaji kwa wanawake na watoto.  Mwandishi wa makala haya alianza safari yake hadi kufika shehia ya Shengejuu Wilaya ya Wete, ambapo alikutana na sheikh Khamis Hamad Nassor alimuelezea kuwa, viongozi wa dini wamekuwa nyuma katika kupinga vitendo vya udhalilishaji katika jamii, kutokana na baadhi yao kujinasibisha kufanya vitendo hivyo. Yeye anaona kuwa, ukemeaji wao ni mdogo ukilinganisha kuwa, hilo ni jukumu lao la kila siku la kuamrishana mema na kukatazana mabaya. “Masheikh na maimamu sisi ndio wasimamizi wakubwa kwa waumini wa kiislamu na ndio tunaosikilizwa na jamii, ingawa baadhi yaetu tumekuwa ni wahusika wa kutekeleza vitendo vya udhalilishaji katika jamii, kutokana kuwa mbele wakati wa sulu

Mkuu wa mkoa ataka madarasa kusakafiwa ili kuepusha vumbi kwa wanafunzi

Image
Na, Haji Nassor Sauti ya Mnyonge, Pemba MKUU wa Mkoa wa kusini Pemba, Hemed Suleiman Abdalla ameliharakisha Baraza la mji wa Chakechake, kuweka saruji chini, kwenye vyumba vinne vya madarasa ya skuli ya msingi Mgelema, ili kuwaepusha na vumbi wanafunzi wanaoyatumia madarasa hayo. Alisema elimu bora haitafutwi kwa mtindo wa wanafunzi kukaa kwenye vumbi, jambo ambalo wanaweza kukosa elimu na hata kupata athari za kiafya kama wakiendelea kuyatumia madarasa hayo. Mkuu huyo wa Mkoa ameeleza hayo skulini hapo, alipokuwa akizungumza na wananchi, waalimu na kamati za wazee wa skuli hiyo, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku moja ya kuikagua miradi nane ya maendeleo, inayoendeshwa na Baraza la mji wa Chakechake. Alisema, lazima juhudi za haraka zichukuliwe na baraza la mji kwa kushirikiana na Kamati husika ya skuli hiyo, ili kuharakisha uwekaji wa saruji, maana wanafunzi wa madarasa ya pili wanaotumia, wanaendelea kuathirika kwa vumbi. Alieleza kuwa, hakuna namna bali ndani ya wiki zisizodi ta