Wananchi wajenga wodi baada ya kuchoshwa na kujifungulia sakafuni
Na Florence Sanawa
Sauti ya Mnyonge, Mtwara
WANANCHI wa Kata ya Mnyeu yenye vijiji vine Wilayani Newala Mkoani Mtwara wamejitosa kujenga wodi na chumba cha kujifugnuliwa baada ya kuchoshwa na udongo wa vyumba hivyo hali ambayo inapelekea wanawake wengi kujifungulia sakafuni.
Ujenzi huo ambao awali ulichangiwa na wakazi wa patao 3455 kwa kutoa shilingi 2000 na baadae kuongezeka kwa kutoa 10000 kwa kila kaya umeleta matuini hali ambayo imemfanya mkuu wa wilaya hiyo Aziza Mangasongo kuchangia mifuko 30 ya saruji ili kukamilisha jengo hilo ambapo mpaka sasa wametumia zaidi ya shilingi milioni 7.
Akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani iliyoadhimishwa kijijini hapo Hawa Akram mkazi wa kijiji hicho alisema kuwa awali walikuwa wa kijifungulia kwenye chumba kidogo chenye vitanda viwili hali ambayo ili kuwa ikiwa weka kwenye hatari zaidi kutokana na wengine kujifungulia chini.
Alisema kuwa kutokana tatizo hilo wanawake wengi wamekuwa wakidharirika hasa wanapotakiwa kujifungua zaidi ya watatu kwa wakati mmoja ambapo wengine hulazimika kutandika nguo chini ili wajifugulie hapo.
“Sio uongo kwa hatua tuliyopiga tumefarijika wanawake tumekuwa tukipata shida wakati wakujifungua tunajifungulia chini kwenye kawodi kadogo kanaako tosha vitanda viwili jambo ambalo linalo sababisha baadhi ya wanawake wadharirike hasa tunapotaka kujifugnua hivi tunawezaje kujifungualia wane ndani ya chumba chenye……….
“Unapokaribia kujifungua unaanza kufikiria jinsi ya kwenda hospitalini hapo kwakweli hali ili kuwa mbaya kitendo cha kila kaya kuchangana kujenga jingo hilo kweli kimetufariji tunaona kuna matumaini kwetu akina mama” alisema Akram
Nae Sharafi Rashid makazi wa kijiji cha Mnyeu alisema kuwa kitendo cha akina mama kujifungulia kwenye sakafu kilikuwa kina wakera hali ambayo ili walazimu wao kupitisha michango ili kuweza kukamilisha jengo hilo.
“Tuliangalia hili jambo na kuamua sisi wenyewe baada ya kuona kero hiyo kwa akina mama kujifungulia sakafuni tulichangana kwa kila kaya shilingi 10,000 ambayo tuliamini kuwa inaweza kutusaidia ambapo tumefanikiwa kujenga jingo hilo …….
“Hatua kuwa tunafurahi kuona akina mama wanajifungulia kwenye chumba kidogo ambacho nafasi yake imebana hali ambayo ili kuwa haipendezi kutokana na mlundikano uliokuwepo kwenye zahanati hiyo hasa wanapo kwenda kujifungua wanawake zaidi ya wawili” alisema Sharafi
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Newala Aziza Mangasongo alisema kuwa wananchi hao wameonyesha ujasiri na ukomavu kwa kushirikiana kutatua matatizo yanayo wakabili.
“Ni kweli zahanati ipo lakini haikidhi mahitaji ya watu wa kata mbili pamoja na halmashauri kuwa mipango mbalimbali kwa kata zake bado tunashuhudia nguvu ya umma ikiwa na mwamko mkubwa zaidi hali ambayo inanivuta na mimi kushirikia nao ili waweze kumalizia ujenzi huo nitatoa mifuko 30 saruji” alisema Mangasongo.
Comments
Post a Comment