Mkuu wa Wilaya aumia wanafunzi wa kike kukatisha masomo

Na, Florence Sanawa
Sauti ya Mnyonge, Tandahimba

 MKUU wa Wilaya ya Tandahimba Mkoani Mtwara Sebastian Waryuba amesema kuwa wilaya hiyo inakabiliwa na tatizo kubwa la wanafunzi wakike kuacha shule wakiwa sekondari kutokana na kupata ujauzito wakiwa na umri mdogo.

Akizungumza wakati wa kampeni ya kupiga vita mimba kwa watoto wakike mashuleni juzi alisema kuwa changamoto hiyo inapelekea kushuka kiwango cha elimu wilayani humo huku watoto wengi wakike wakiwa katika hatari zaidi kutoana na mimba za utotoni.

Alisema kuwa shule za sekondari zinaongoza kwa wanafunzi kuacha shule hali ambayo ambayo serikali imezindua kampeni ikiwa ni mkakati ili kuweza kukomesha tatizo hilo ambalo limekuwa likikatisha ndoto za wanafunzi wengi wilayani humo.

“Kwa sehemu kubwa kumekuwa na tabia ya wazazi kukaa na kukubaliana wakati wa ujauzito wa mtoto hali ambayo inawafanya wawe na sababu nyingi kuliko maelezo jambo ambalo linapelekea wialya kurudi nyuma kielimu……..

“Ili tuweze kufikia uchumi wa kati na kuifanya Tanzania iwe ya viwanda msukumo kwa wanawake unatakiwa ili waweze kusoma hawa watoto wa kike ni akina mama wa baadae ambao wanapaswa kuungwa mkono ili waweze kutimiza ndoto zao” alisema Waryuba

Nae Afisa Maendeleo ya Jamii Mkuu wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wazee na Watoto kutoka Idara ya Maendeleo ya Watoto Christopher Mushi  alisema kuwa kampeni hiyo ni ya kitaifa ambayo ilizinduliwa hivi karibuni mkoani Mara.

“Hii ni kampeni ya kitaifa tunaenda mkoa kwa mkoa ambayo imeanzia mkoani Mara ambapo tumeona mwitikio ni mkubwa sana tunaamini kuwa tukiungana kwa pamoja tunaweza kufanikiwa…….

“Mwaka 2016 Tanzania bara zaidi ya wanafunzi Elfu 533 wa shule za sekondari na msingi ndio walioacha shule ambapo katika mikoa iliyoathirika sana ni katavi 45 tabora 43, shinyanga 41, Mara 37 ndio inayoongoza kwa wanafunzi kuacha shule” alisema Mushi

Nae Mwakilishi wa Afisa Elimu wa Wilaya hiyo Hilda Hinjo alisema kuwa watoto wengi wamekuwa wakijihusisha na vietndo vya ngono katika umri mdogo.

Alisema kuwa ipo mikakati ambayo halmashauri imeweka ili kukabiliana na tatizo la mimba ikiwemo kuwajengea uwezo walimu wa kike ili waweze kuwa na urafiki wa karibu ambao unaweza kuwapa hamasa watoto wa kike kusoma.

“Vipo vikundi vya walimu vimeundwa ili kuweza kuendeleza hii kampeni mashuleni ili tuweze kukabiliana na tatizo la mimba mashuleni  ndio maana tunaweza kusema kuwa tunataka tuwe na kauli moja ili mtoto aweze kusoma hatutaki mimba kwa mtoto wa kike ili aweze kuwa na mazingira bora katika elimu” alisema Hinjo

Comments

Popular posts from this blog

Wananchi wajenga wodi baada ya kuchoshwa na kujifungulia sakafuni

Sita wapotea katika mazingira tatanishi wilayani Wete

Jaji Mkuu Zanzibar awashukia mahakimu wanaonyanyasa watuhumiwa