Kiwango kidogo cha ufaulu wa mitihani chamtia wasi wasi mkuu wa mkoa
MKUU wa Mkoa wa kusini Pemba, Hemed Suleiman Abdall amesema, amekiri kutoamini sababu ya wilaya ya Mkoani kutofanya vyema kwenye mitihani ya taifa kwamba kumechangiwa na uhaba wa waalimu, bali ana mashaka na hamu na ari ya ufundishaji wa baadhi ya waalimu hao. Alisema anashangaa kuona baadhi ya skuli kama Mizingani sekondari na nyengine pana masomo hayana waalimu, ingawa ufuaulu wake ni mkubwa ukilinganishwa na yale masomo kama ya dini, Kiswahili na kiarabu ambayo yanawaalimu wa kutosha lakini ufaulu wake ni mbovu, Mkuu huyo wa Mkoa, ameeleza hayo skuli ya Mohamed Juma Pindua, alipokuwa akizungumza na waalimu wakuu, wa msingi, sekondari na wenyeviti wa kamati zao, kwenye mkutano wa kutathimi, kufuatia wilaya hiyo kutofanya vyema kwenye mitihani ya taifa iliopita. Alisema, yeye binafsi anamashaka na aria na hamu ya waalimu iwapo wanajua wanchokifanya wanapokuwa madarasani bali kuna jambo jengine, ambalo lilisababisha ubovu wa matokeo hayo ya taifa na sio uhaba wa waalimu pe...