Wadau wataka ZBC iwezeshwe kushindana kihabari na luninga zingine

Na, Haji Nassor
Sauti ya Mnyonge, Pemba

WADAU wa habari kisiwani Pemba, wameishauri Wizara ya Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo Zanzibar, kuendelea kujipanga vyema, ili Shirika la Utangaazaji Zanzibar ZBC liwezea kuingia katika soko la ushindani wa kihabari.

Walisema shirika hilo kupitia tv yake ya rangi, ililianza mwanzo barani Afrika kwenye mwaka 1973, lakini linashindwa kwenda sambamba na vyombo vyengine ya habari, na kupoteza watazamaji.

Wakizungumza kwenye mkutano wa kutafuta maoni kwa wadau juu ya kuimarisha utendaji wa kazi kwa vyombo vya habari ya serikali, uliofanyika uwanja wa michezo wa Gombani Chake chake kisiwani humo, walisema bado shirika hilo linamtihani mitambo yake.

Walisema ni aibu kwa sasa kuona shirika hilo la utangazaji kupitia tv, vipindi na matangaazo yake yatabia ya kukata kata na wakati na mwengine kuzima kabisa na kuwakosesha raha watazamaji wake.

Mmoja kati washiriki wa mkutano huo, sheha wa shehia ya Mkoroshoni Khamis Iddi Songoro, alisema yeye hujipanga vyema kufuatilia hutuba za viongozi, ingawa haimaliziki posi na kujitokeza mistari.

“Ushafungu ZBC, unaangalia hutuba ya kiongozi au kipindi maalum, kidogo unaona rangi za mikeka mikake au kiza na wakati mwengine, unaona picha husikii sauti,”alieleza.

Nae mjumbe kutola Klabu ya waandishi wa habari Pemba PPC, Ali Mbarouk Omar, alisema bado shirika hilo ambalo ni kongwe kwa ukanda wa Afrika Mashiriki, lijipange vyema ili lisikikimbiwe na watazamaji.

Kwa upande wake Sheha wa shehia ya Selemu Ali Khatib Chwaya alisema, wakati mwengine kinachojitokeza ndani ya ZBC, ni kuchelewa kwa dakika 10 hadi 15 kuanza kwa kipindi husika.

“Unaweza kukaa kwenye redio au tv unasubiri kipindi, pengine kinatakiwa kianze saa 3:15, lakini inakwenda hadi saa 3:30 ndio kinaanza na hilo ndio mara nyingi sio bahati mbaya,”alieleza.

Katika hatua nyengine, wadau hao wakiwemo waandishi wa habari, walisema changamoto kubwa wanayokumbana nayo, ni kutakiwa kuomba kupatiwa habari kwa njia ya barua, jambo ambalo linawapa shida.

Mwandishi kutoka Idara ya Habari Maelezo Pemba Mohamed Khalfan Ali , alisema inashangaa kuona baadhiya tasisi tena za serikali, zimekuwa na urasimu mkubwa unapohitaji habari.

“Kwa sasa afadhali wenzetu wa Jeshi la Polisi, wanaushirikiano mzuri, lakini tasisi nyengine ukihitaji kupata habari ya kuwaelimisha wananchi, uombe kibali cha Katib Mkuu wa wizara husika,”alieleza.

Nae Kauthar I-shaka alisema, hata unapohitaji kufanya vipindi kwenye hospitali na skuli mbali, wakuu wa taasisi hizo, wamekuwa wakivaa majoho ya kukataa kuzungumza na waandishi wa habari.

Mapema Afisa Mdhamini wizara ya Habari Pemba, Khatib Juma Mjaja alikiri kuwepo kwa tatizo kwenye shirika la utangaazaji Zanzibar, ingawa serikali imekuwa mstari wa mbele kutatua hatua kwa hatua.

Hata hivyo alisema, kwa sasa wizara ya Habari imekua ikijitahidi kuondoa changamoto kadhaa, na ndio maana imetumia gharama kubwa, kufunga vifaa vipya.

Mkurugenzi Mipango, Sera na Utafiti wa Wizara hiyo Zanzibar Mahamoud Omar Hamad, alisema kutokana na michango ya wadau, hao, wamefarajika kutokana na kuwepo kwa mambo kadhaa ya kufuatilia.

Huu ni mkutano wa kwanza kuandaliwa na Wizara ya Habari Zanzibar, wa kujumuisha wadau, kwa ajili ya kuchukua maoni yenye lengo la kuimarisha utendaji wa kazi.

Comments

Popular posts from this blog

Wananchi wajenga wodi baada ya kuchoshwa na kujifungulia sakafuni

Sita wapotea katika mazingira tatanishi wilayani Wete

Jaji Mkuu Zanzibar awashukia mahakimu wanaonyanyasa watuhumiwa