Kaya zaidi ya elfu tatu hatarini kwa magonjwa ya mlipuko Kagera




Kaya 4,364, zipo hatarini kukumbwa na magonjwa ya milipuko wilayani Misenyi mkoani Kagera, kutokana na kutokuwa na vyoo na kuvitumia.

Hayo yameelezwa na mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Missenyi Bw. LIMBE BENARD,  wakati akizungumza na mwandishi wa mtandao huu juu ya mkakati kwa kaya zisizo na vyoo, ilhali zina mahitaji ya miundombinu hiyo muhimu.

Amesema kuwa  takwimu hizo zimebainika katika mchakato wa kutambua vyoo bora kila kaya, uliofanyika katika mwezi January mwaka huu 2018, kwa kuhusisha jumla ya kaya 37,685 zilizokaguliwa na kuhojiwa kwa wanakaya wenyewe.

Bw. LIMBE ameongeza kuwa katika utambuzi hu, zipo kaya ambazo zimekubali na kuanza uchimbaji na ujenzi wa vyoo, ingawa kaya 102 kati ya hizo zimekaidi kufanya hivyo, na kuilazimu serikali kuzitoza faini ya jumla ya shilingi laki 6 na elfu 50.

Pamoja na kutozwa faini hizo, imeelezwa kuwa wanaendelea kufatiliwa kwa lengo la kujihakikishia kama wametekeleza agizo ili kuepusha kuwasababishia wengine matatizo ya kiafya. 

Mkakati wa serikali juu ya hali hiyo,  Bw. LIMBE alisema kuwa, halmashauri yake inaendelea kutoa elimu juu ya umuhimu wa choo, na kueleza madhara yanayotokana na ukosefu wake, baada ya kubaini baadhi ya wananchi kushindwa kuelewa umuhimu wa choo bora ya kutumia.

Baadhi ya wananchi wasio na vyoo waliozungumza na mtandao huu, walikiri kutokuona sababu za kulazimishwa kuwa choo, kwani wana uwezekano wa kujisaidia vichakani kama ambavyo wamekuwa wakifanya kwa mujibu wa maelezo yao.


Comments

Popular posts from this blog

Wananchi wajenga wodi baada ya kuchoshwa na kujifungulia sakafuni

Sita wapotea katika mazingira tatanishi wilayani Wete

Jaji Mkuu Zanzibar awashukia mahakimu wanaonyanyasa watuhumiwa