Wanasheria Pemba watembelea shule mbalimbali kuadhimisha siku ya sheria Zanzibar

Picha na Maelezo, Haji Nassor
Sauti ya Mnyonge, Pemba

WANAFUNZI wa skuli ya Ufundi Kengeja wilaya ya Mkoani Pemba, wakifuatilia mkutano wa elimu ya sheria, iliotolewa na wanasheria mbali mbali waliofika skulini hapo, ikiwa ni sehemu ya shamra shamra za kuelekea siku ya sheria Zanzibar, kamati hiyo ilikuwa chini ya Mwenyekiti wake Mhe: Hussein Makame Hussein

MRAJISI wa mahakamu kuu Jimbo Pemba, Mhe: Hussein Makame Hussein, akijibu masuali mbali mbali ya wanafunzi wa skuli ya Ufundi Kengeja, wakati Kamati ya maandalizi ya sherehe ya siku ya sheria Zanzibar, ilipofika skulini hapo, kutoa elimu ya sheria

BAADHI ya watendaji wa mahakama kisiwani Pemba, wakifuatilia mkutano wa kutoa elimu ya sheria, kwa wanafunzi wa skuli ya ufundi Kengeja wilaya ya Mkoani

MWANASHERIA wa serikali na Mwendesha Mashitaka kutoka ofisi ya DPP, Ali Haidar Mohamed akizungumza kwenye mkutano wa elimu ya sheria, kwa wanafunzi wa skuli ya Ufundi Kengeja, ambapo ni shamra shamra za kuelekea siku ya sheria Zanzibar


HAKIMU wa mahakama ya Ardhi Chakechake, Salum Hassan Bakar, akifafanua jambo kuhusu matumizi ya ardhi kwenye mkutano huo, uliofanyika skuli ya Ufundi Kengeja.

MARTIBU wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba, Fatma Khamis Hemed, akielezea kazi za kituo hicho, mbele ya wanafunzi wa skuli ya Ufundi Kengeja, kwenye mkutano wa elimu ya sheria kuelekea siku ya sheria Zanzibar.

Comments

Popular posts from this blog

Wananchi wajenga wodi baada ya kuchoshwa na kujifungulia sakafuni

Sita wapotea katika mazingira tatanishi wilayani Wete

Jaji Mkuu Zanzibar awashukia mahakimu wanaonyanyasa watuhumiwa