DC Tandahimba aamua kukomalia mimba kwa wanafunzi
Na Florence Sanawa Sauti ya Mnyonge, Mtwara KUFUATIA kuwepo kwa tatizo kubwa la ujauzito kwa shule za sekondari Wilayani Tandahimba ambapo katika ripoti ya mwaka 2017 imeonyesha kuwa zaidi ya wanafunzi 55 wameacha shule kutokana na tatizo hilo. Hali hiyo imeilazimu kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ikishirikiana Mkuu wa Wilaya hiyo Sebastian Waryoba kufanya msako ili kuwabaini wanafunzi hao shule wanazotoka na kuwafahamu wazazi wao ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa. Kauli hiyo ameitoa juzi wakati wa kikao cha ushauri cha halmashauri ya wilaya hiyo (DCC) ambapo baada ya kutopokea taarifa ya elimu iliyosomwa na afisa elimu sekondari sostenes luhende alisema kuwa taarifa hiyo imemshtua hivyo kutaka kujua hatua zilizochukuliwa baada ya wanafunzi hao 55 kuacha shule kutokana na ujauzito. Alisema kuwa kulingana na taarifa hiyo alisema kuwa lazima hatua zichukuliwa haraka ili iwe fundisho kwa wengine hatua ambayo inaweza kupunguza tatizo la mimba wilayani humo. Waryoba alisema...