TAFITI: Pembejeo za bure hazikunufaisha wakulima wa korosho Tandahimba

Florence Sanawa,
Sauti ya Mnyonge, Kanda ya Kusini

WAKULIMA Wilayani Tandahimba wameiomba serikali kufanya sensa ya mikorosho ili kuondoa changamoto zilizojitokeza katika msimu wa 2017/18 ambapo wakulima wengi hawakupata pembejeo za bure zilizotolewa na serikali.

Akitoa takwimu hizo Mtafiti kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam Messia Illomo alisema kuwa katika utafiti uliofanywa kwa baadhi ya maeneo wilayani humo ulibaini kuwa katika msimu huu wakulima wametumia gharama kubwa zaidi kuliko misimu yote iliyopita.

 “Tulibaini kuwa ni kweli serikali ilitoa pembejeo bure lakini kwa kiasi kikubwa wakulima wamenunua kuliko walizopewa bure pia zilichelewa na zingine zilikuja kwa awamu ya mwisho ambapo ilichelewa sana”

“Ujio wa peembejeo kwa awamu kumezua migogoro ya hali ya juu kwa wakulima kwakuwa ilifikia hatua ya kugombana na kufikishana kwenye vyombo vya sheria…..

“Lakini pia Bodi ya korosho Tanzania (CBT) iangalie uhahlisia ili kuendana na wakulima wapo wakulima wanasema kuwa pembejeo zilizoletwa hazina ubora mvua ikinyesha zinadondoka kwenye ardhi jambo ambalo linapelekea wakulima kuikataa dawa hiyo”

Kwa upande wake mkulima kutoka Kata ya Mchichira Wilayani Tandahimba Asha Walambo alisema kuwa utoaji wa pembejeo ya bure imeathiri wakulima kwa kiasi kikubwa.

“Yaani mimi kama mkulima ningeshirikishwa juu ya utoaji wa pembejeo bure wala nisingekubali kwakuwa bure ina gharama hata ukiangalia sehemu kubwa walionufaika sio wakulima wapo waliotumia nguvu ili kupata dawa hiyo ni bora tungeendeelea kuapata pembejeo ya ruzuku”  

Comments

Popular posts from this blog

Wananchi wajenga wodi baada ya kuchoshwa na kujifungulia sakafuni

Sita wapotea katika mazingira tatanishi wilayani Wete

Jaji Mkuu Zanzibar awashukia mahakimu wanaonyanyasa watuhumiwa