Wananchi wataka eneo la barabara lililokatika lijengwe daraja

Na Haji Nassor
Sauti ya Mnyonge, Pemba

MADEREVA na wananchi wanaotumia barabara ya Mkoani- Chakechake, wamesema wakati umefika wa wizara husika ya ujenzi wa barabara, kujenga daraja maalum eneo la Changaweni Mkoani, kufuatia kuharibika tene eneo ambalo lilijegwa hivi karibuni na wizara hiyo.

Walisema, ishara zinaonyesha eneo hilo asili yake ni kuwepo kwa mto unaokatisha chini kwa chini, na ndio maana kila mvua zinaponyesha, hujitokeza uharibifu.

Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi kwenye eneo hilo, walisema wanashangaa kuona miezi mitatu, iliopita wizara husika ilitumia gharama kubwa kujenga eneo hilo, na tayari mvua ilionyesha juzi, pameshaharibika tena.

Mwananchi Hamad Khamis, alisema awali juzi hiyo alipopita alishuhudia ufa mkubwa ulipakana na barabara kongwe, na baadae majira ya mchana alionona hali kuongezeka.

“Hata sisi wapiti njia hii hali inatutia wasi wasi, maana hutujui wakati gani inaweza kukatika, na kila mtu na wa umri wote wanapita hapa, lazima pajengwe daraja”,alishauri.

Nae Mbwana Juma (55), alisema eneo hilo kwa ufahamu wake, anakumbuka palikua na mto na wakati barabara hiyo inajengwa wakati wa rais Amani, walipafukia badala ya kujengwa daraja.

“Mimi kwa uzee wangu, naelewa hapa palikuwa na daraja, saa kama wizara husika inafukia mawe, mpasuko maisha itakuwa hauondoki, maana maji yanapenya chini kwa chini”,alifafanua.

Dereva wa gari ya mzigo, Omar Khamis, alisema eneo hilo siku zote hupita na wasiwasi wa maisha yao, hasa gari inapokuwa na mzigo.

“Gari ikiwa na mzigo huzidi uzito, sasa lazima eneo hili kwa vile pameshaonyesha athari ya mara kwa mara kila mvua inaponyesha, pajengwe daraja”,alisema.

Kwa upande wake Afisa Mdhamini wa wizara inayoshughulikia ujenzi wa barabara Hamad Ahmed Baucha, alisem kwanza wanahangaika kupelekea vifaa, ili kuirejesha hali yake.

Alisema baada ya kupata taarifa hiyo juzi Disema 10, aliwaarifu watendaji wake, na walikwenda kupangaalia ili waanze hatua ya kufanya matengenezo.

Aidha ameendelea na wito wake wa kuwataka wananchi kuendelea kutoa taarifa za haraka, wanaposhuhudia barabara hiyo, kuanza kuharibika.

Mvua ilionyesha miezi mitano iliopita, iliripotiwa kutokezea kwa uharibifu mkubwa wa miundombinu ikiwemo kuharibika kwa barabara, madaraja na milima kuporomoka hali iliosababisha uharibifu mkubwa.

Comments

Popular posts from this blog

Wananchi wajenga wodi baada ya kuchoshwa na kujifungulia sakafuni

Sita wapotea katika mazingira tatanishi wilayani Wete

Jaji Mkuu Zanzibar awashukia mahakimu wanaonyanyasa watuhumiwa