DC Tandahimba aamua kukomalia mimba kwa wanafunzi

Na Florence Sanawa
Sauti ya Mnyonge, Mtwara

KUFUATIA kuwepo kwa tatizo kubwa la ujauzito kwa shule za sekondari Wilayani Tandahimba ambapo katika ripoti ya mwaka 2017 imeonyesha kuwa zaidi ya wanafunzi 55 wameacha shule kutokana na tatizo hilo.

Hali hiyo imeilazimu kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ikishirikiana Mkuu wa Wilaya hiyo Sebastian Waryoba kufanya msako ili kuwabaini wanafunzi hao shule wanazotoka na kuwafahamu wazazi wao ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa.

Kauli hiyo ameitoa juzi wakati wa kikao cha ushauri cha halmashauri ya wilaya  hiyo (DCC) ambapo baada ya kutopokea taarifa ya elimu iliyosomwa na afisa elimu sekondari sostenes luhende alisema kuwa taarifa hiyo imemshtua hivyo kutaka kujua hatua zilizochukuliwa baada ya wanafunzi hao 55 kuacha shule kutokana na ujauzito.

Alisema kuwa kulingana na taarifa hiyo alisema kuwa lazima hatua zichukuliwa haraka ili iwe fundisho kwa wengine hatua ambayo inaweza kupunguza tatizo la mimba wilayani humo.

Waryoba alisema kuwa katika kipindi cha mwaka mmoja kufukuza wanafunzi 55 kwa kupata ujauzito hiyo ni aibu kubwa hivyo kutaka wazazi, wanafunzi wote kukamatwa ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa haraka iwezekanavyo ili kuweza kudhibiti tatizo hilo.

“Unajua sio jambo rahisi kulifumbia macho ndio maana nataka nijue ni akina nani walioacha shule walitoka shule gani, wazazi wao ni akina nani waliowapa ujauzito hatua gani za kisheria  zilichukuliwa taarifa zote zije kwangu hata kama alishaachaga shule miaka miwili iliyopita nataka kujua alikuwa na umri gani naagiza wote wakamatwe”  


Miezi michache iliyopita mkuu wa mkoa wa mtwara gellasius byakanwa alishangazwa na taaria ya kikao cha wadau wa elimu ambapo kikao hicho cha mkoa kilionyesha kuwa wanafunzi zaidi ya 393 wa shule za sekondari wamepata ujauzito katika kipindi cha miaka mitatu huku wilaya ya Tandahimba pekee ikiongoza kwakuwpo kwa tatizo hilo.

Comments

Popular posts from this blog

Wananchi wajenga wodi baada ya kuchoshwa na kujifungulia sakafuni

Sita wapotea katika mazingira tatanishi wilayani Wete

Jaji Mkuu Zanzibar awashukia mahakimu wanaonyanyasa watuhumiwa