WATOTO WENYE ULEMAVU WA AKILI MTWARA WASHIRIKISHWE KATIKA MICHEZO
Watoto wenye ulemavu wanapaswa kupewa kipaumbele katika michezo ili kuweza kufanikisha adhima ya kuwajenga kiakilia na kuwafanya wawe na uelewa zaidi katika mambo mbalimbali.
Uelewa huo huwafanya wafahamu mambo mbalimbali hali ambayo huchangia kuwaweka karibu na jamii isiyo na ulemavu hivyo kupata uelewa zaidi hasa wanapo changamana.
Watoto hao ambao hushiriki michezo mbalimbali katika na fanikisha kufika katika ngazi ya kitaifa wamekuwa na hali na mori ya kutaka kujua vitu vingi ili waweze kushiriki kikamilifu na wenzao wasio na ulemavu katika michezo ikiwemo kukimbia, kuruka kamba na michezo mingine mingi.
Afisa elimu maalum manispaa ya mtwara mikindani Ally Ndale anasema kuwa watoto wenye ulemavu wa akili wanapaswa kushirikishwa katika michezo mbalimbali ili kuwachangamsha na jenga.
“Watoto wenye ulemavu wa akili huwa wanajifunza taratibu sana ndio maana tunawafundisha kwa njia ya Michezo hii inawajenga kiakili ili kuwaweka katika mazinginra mazuri na kuangalia uwezo wao kiakili na kuwachangamsha kutokana na ulemavu walionao” alisema Ndale
Nae mratibu wa michezo Special Olympic mkoa wa mtwara Andrea magani alisema kuwa michezo hiyo imefanyika maalum kwaajili ya kuwaandaa watoto wenye ulemavu wa akili wenye umri wa miaka 2-7.
“Michezo hii inawakuza kiakili mtoto mwenye ulemavu wa akili anajifunza kwakutumia michezo ndio maana tunawafundisha sheria na kanuni ili waweze kuishi vizuri na jamii katika michezo tunaweza kumfundisha mtoto jinsi ya kuishi” alisema Magani
Comments
Post a Comment