Mtwara na Lindi mbioni kuingia kwenye gridi ya Taifa

Florence Sanawa,
Sauti ya Mnyonge, Kanda ya Kusini

Kutokana na kuwepo kwa tatizo kubwa la kukatika kwa umeme katika mikoa ya lindi na mtwara Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) imesema kuwa mikoa ya Lindi na Mtwara iko njiani kuingia katika grid ya Taifa ambapo itasaidia kutatua tatizo la umeme lililopo katika mikoa hiyo.  

Akizungumza wakati wa ziara yao iliyofanyika jana Mkoani Mtwara Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi wa shirika hilo Alexander Kyaruzi  alisema kuwa mikoa hiyo itaingia kwenye grid ya taifa baada ya ujenzi wa laini ya kilovoti 400 kutoka mtwara hadi somanga fungu na somanga fungu  hadi kinyerezi kilovote 

Alisema kuwa tatizo lililopo hivi sasa linaweza kutatulika kwa kuunganishwa kwenye huo mtambo mkubwa wa umeme ambao ndio unatumiwa na mikoa mingi hapa nchini.  

“Hili tatizo la uemme litaisha wakiingia kwenye grid ya taifa ambapo mtambo mmoja utakuwepo Mtwara na mwingine utakuwepo somanga fungu hili ndio litakuwa suluhisho kwa mikoa ya lindi na mtwara kupata umeme wa uhakika hadi kufikia 2020” 

“Serikali imefanya mazungumza na serikali ya Japani kupitia shirika lake la JAICA kwa ajili ya kujenga mitambo ya kufua umeme wa megawati 300 kwa mkoa wa Mtwara ili waweze kuondokana na tatizo hilo……. 

Wakazi wa mikoa ya Lindi na Mtwara walipata adha hiyo kwa kipindi cha muda wa miezi mitatu hivyo kukamilika kwa ujenzi wa kiwanda hicho kitaweza kupunguza matatizo ambayo yalikuwa yanawakabili katika kipindi hicho” 

“Bodi ya wakurugenzi imekuja kuangalia changamoto ambazo inaikabilia tanesco ili waweze kuangalia namna bora itakavyoweza kujipanga kuhakikisha mikoa hii haitapitia tena katika wakati mgumu wa tatizo la umeme.” Alisema  

Pia alisema kuwa Mikoa hiyo ipo katika mpango wa kuingizwa katika mtambo mkubwa unaogawa umeme nchini (grid ya taifa) ambapo kwa sasa wanatarajia kujenga

Comments

Popular posts from this blog

Wananchi wajenga wodi baada ya kuchoshwa na kujifungulia sakafuni

Sita wapotea katika mazingira tatanishi wilayani Wete

Jaji Mkuu Zanzibar awashukia mahakimu wanaonyanyasa watuhumiwa