WANYONGE 3,647 NANYUMBU WANUFAIKA BWAWA LA MAJI SENGENYA

WAKAZI zaidi ya 3,647 wa vijiji vinne vya Sengenya, Mara, Matimbeni na Ngalinje Wilayani Nanyumbu Mkoani Mtwara wamenufaika na huduma ya maji safi na salama kutoka katika bwawa la kuvunia maji lilitengenezwa na Halmashauri hiyo kutokana na shida kubwa ya maji iliyopo Wilayani humo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu Hamis Damumbaya anasema kuwa ubunifu wa mradi huo ulitokana na uhaba mkuwa wa maji unaikabili Halmashauri hiyo.

 Tunapoendelea kuongeza miradi kama hii ambayo inasimamiwa na jamii yenyewe mbali na kutatua tatizo la maji pia inatatua tatizo la ajira kwa vijana wanaosimamia na kuuza maji hayo hadi sasa kuna maeneo 16 yanayotoa maji moja kwa moja utaona vijana idadi hiyo pia wametapa ajira……

“Unajua serikali imetutaka kuwashirikiana na wananchi pindi wanapoibua miradi kama hii inapokamilika tunawaachia wenyewe waendeshe  hata katika ulinzi wa miundombinu hiyo wamekuwa mstari wa mbele kulinda ikiwemo kulinda mazingira ya bwawa hilo ambalo limekuwa likiwasaidia kwa kiasi kikubwa” alisema Damumbaya

mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya nanyumbu

Nae  Asha Issa Mkazi wa kijiji cha Mara alisema kuwa ujio wa huduma ya maji umeongeza furaha kwa wanawake na watoto kwakuwa wameacha kukesha kwenye visima hali ambayo ilikuwa ikijitokeza hapo awali.

"Sisi tuna lala kwa amani tunaamka kwa amani kwkauwa huduma ya maji ipo mlangoni sina shaka ila naomba serikali iwasaidie wananchi wengine ambao hawapati huduma ya maji wanatembea umbali mrefu na wengine wakipoteza ndoa zao wasaidiwe ili kunusuru hatari kubwa zinazotokea wakati ambao maji hakuna kwenye familia”alisema Issa

Comments

Popular posts from this blog

Wananchi wajenga wodi baada ya kuchoshwa na kujifungulia sakafuni

Sita wapotea katika mazingira tatanishi wilayani Wete

Jaji Mkuu Zanzibar awashukia mahakimu wanaonyanyasa watuhumiwa