Waziri aziagiza tafiti zaidi ili kuongeza uzalishaji wa mbegu

Na Florence Sanawa & Marry Sanyiwa
Sauti ya Mnyonge, Kanda ya Kusini

NAIBU Waziri wa Kilimo Dk Mary Mwanjelwa ameziagiza taasisi zinazojishughulisha na utafiti wa mbegu nchini kuongeza uzalishaji wa mbegu bora ili kukidhi mahitaji ya wakulima nchini. 

Kauli hiyo ameitoa juzi wakati alipotembelea Taasisi ya Utafiti wa kilimo Naliendelea ambapo alisema kuwa uzalishaji wa mbegu kwa wingi unaweza kuhamasisha wakulima kuongeza mazao zaidi.  

Alisema kuwa taasisi zinazo fanya utafiti nchini zinapaswa kuongeza juhudi ili wakulima wanufuaike na tafiti hizo ambazo zimekuwa zikiwanufaisha wakulima wachache zaidi hivyo kuto nufaika na tatifi hizo hivyo kushindwa kuzalisha kwa tija. 

Dk Mwanjelwa alisema kuwa endapo vituo vingi vya utafiti vitazalisha mbegu kwa tija vinaweza kuwasaidia wakulima wengi ambao wanaweza kupata mbegu hizo kwa urahisi hivyo kuongeza uzalishaji nchini.  

“Zipo taasisi nyingi kwenye taasisi zingine za utafiti wa kilimo wajiongeze kama taasisi ya NALIENDELE wanavyofanya kuhakikisha kwamba wanakuwa na ubunifu zaidi na wanatoa mbegu bora licha ya asa ambayo ni taasisi ya kiserikali pia ihakikishe inauza mbegu hizo zinauzwa kwa bei ambayo mkulima atamudu kuinunua mbegu hiyo………

“Naona katika taarifa yenu mmesema mmeweza kufanya tafiti na kufanikiwa kupata korosho bora ya W130 ndio pekee duniani tunapaswa tuijulishe dunia kuwa aina hii inapatikana nchini kwenye kituo chetu cha utafiti NALIENDELE mambo mazuri ukiyanyamazia hakuna mtu atakaejua haya ndio manufaa ya kituo chetu cha utafiti”

“Andikeni maandiko mbalimbali ndio maana ya kuwa watafiti tumieni utalaamu wenu ili muweze kupata fedha kutoka katika taasisi mbalimbali kwa sababu sekta ya kilimo kila mmoja anapenda kuweka fedha zake pia ni sekta ambayo imeshika maisha ya watanzania” 

“Hata hawa Maafisa ugani hakikisheni wapewa elimu yakutosha kupitia mashamba darasa ili elimu hii iweze kuwafikia wakulima na kuwanufaisha na tafiti zinatolewa na taasisi hiyo, Maisha ya Mtwara ni korosho ambapo ni asilimia 60 hakikisheni kuwa mnaongeza kwa sasa ni asilimia 40 mazao mengine haitoshi ili kuwepo kwa mazao mengine ili muweze kufanya kitu kizuri zaidi lazima mtoke ili wakulima wajivunie utafiti wenu na ubora zaidi wenye ufanisi kwa wakulima” Dr Mwanjelwa

Comments

Popular posts from this blog

Wananchi wajenga wodi baada ya kuchoshwa na kujifungulia sakafuni

Sita wapotea katika mazingira tatanishi wilayani Wete

Jaji Mkuu Zanzibar awashukia mahakimu wanaonyanyasa watuhumiwa