Wazazi watakiwa kufichua watoto wenye maradhi ya moyo
Na, Haji Nassor Sauti ya Mnyonge, Pemba WAZAZI na walezi wa watoto wenye maradhi ya moyo Zanzibar, wametakiwa kuwafichua watoto wao, na kuwapeleka katika kliniki za hospotali za serikali, ili kufanyiwa uchunguuzi na kisha kupatiwa matibabu ya haraka. Ushauri huo umetolewa na aliekuwa mgonjwa wa mwanzo Zanzibar kufanyiwa operesheni mbili ndani ya mwezi mmoja nchini Is-rail mwaka 1999 Arafa Abdulla Ali alipokua akizungumza na mwandishi wa habari hizi kisiwani Pemba. Alisema ugonjwa wa moyo unatibika na unapona na kurudi katika hali ya kawaida, hivyo hakuna sababu kwa wazazi au walezi kuwavundika ndani watoto wao. Alisema serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia wizara yake ya Afya, imekuwa na ushirikiano mzuri wa kimatibabu na nchi za India na Is-rail, hivyo kwa sasa wazazi hawana sababu ya kuogopa gharama za matibabu, kwa vile hilo hubebwa na nchi husika. Alieleza kuwa, yeye alifanikiwa kupona maradhi hayo ya moyo kutokana na wazazi wake, kumfikisha mapema hospitali ya Mnazi mmoja...