Madereva wasiozingatia vivuko vya watembea kwa miguu wachukuliwe hatua kali
Imeandaliwa na, Shushu Joel BARABARA ni msingi mkubwa katika nchi kwa ajili ya kupiga hatua ya maendeleo katika taifa lolote duniani. Kila nchi inahitaji kuwa na barabara nzuri ili kufanikisha malengo ya kufanya shughuli zote za usafirishaji wa haraka kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingie pasipo kuwepo na kikwazo cha aina yeyote ile. Katika barabara nyingi kuna alama mbalimbali zinazonyesha ishara ya kitu fulani kwa lengo la kuwasaidia waendeshaji wa vyombo vya moto kama vile magari, pikipiki, baiskeli na vingine vingi ambavyo vinatumia barabara kama njia ya usafirishaji. Alama za barabarani ziko nyingi na zote zikiwa na maana zake na zinatakiwa kufuatwa ili kuzuia ajali,kuna alama za pundamilia ambazo huonyesha kuwa mwenye chombo cha moto anatakiwa kusimamisha gari lake ili watembeao kwa miguu kuweza kupita bila usumbufu wa aina yeyote ile. Lakini kwa madereva walio wengi wanashindwa kufuata sheria za barabarani kwa kisingizio cha kupoteza muda,hivyo hawasimami kwenye pundamilia il...