Waomba mbadala wa mkandarasi kunusuru hali tete ya ubovu wa barabara.

Na, Mack Ngaiza
Sauti ya Mnyonge, Kanda ya Ziwa

Wakaazi wa kata ya Kahoroho na watumiaji wa barabara ya mjini Bukoba-Mugeza, wameendelea kushangazwa na kukwama kwa ujenzi wa barabara hiyo inayosababisha adha kubwa kwa shughuli za kibinadamu.

Pamoja na ubovu wa barabara hiyo hatua zilizojadiliwa tangu miaka 4 iliyopita na kupitishwa katika vikao vya baraza la madiwani hazijazaa matunda kwa sababu ambazo wananchi hawazielewi, na kutokana na hali hiyo mwenyekiti wa bodi ya wakala wa barabara mjini na vijijini na kaimu katibu tawala mkoani Kagera, wametakiwa kufuatilia uongozi wa manispaa ili kujua kwanini mkandarasi hakufika kusaini mkataba kwa muda uliopangwa.

Akizungumza kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Kagera, mkuu wa wilaya ya Bukoba Deodatus Kinawilo, wakati wa kusainishwa mikataba kwa wakandarasi ambao amepata tenda za kutengeneza barabara, amesema kuwa ameshangazwa na manispaa kushindwa kusainisha mkataba wao kwa madai kwamba mkandarasi anasafiri.

Amesema kuwa haiwezekani mkandarasi huyo akatae kufika kusaini mkataba kwa muda uliopangwa, na ikizingatiwa waliokuwa wameomba kazi hiyo walikuwa wengi na tayari serikali imeshatafuta fedha kwa ajili ya manispaa jumla ya shilingi bilioni 7.44 , hivyo kuna mashaka juu ya upatikanaji wa mkandarasi huyo.

Kaimu mkurugenzi manispaa ya Bukoba Chibhunu Lukiko, amesema kuwa manispaa ilikuwa imekubaliana Februari 1 kumsainisha mkataba mkandarasi ambaye ni Mwananchi Engineering Company –MAECO, ambapo pamoja na mkuu wa wilaya kumtaka afike kusaini mkataba februari 2 mwaka huu, hakufika kusaini.

Amesema kuwa mkandarasi huyo amesema kuwa hasingeweza kufika terehe hiyo kwani ameishakata tiketi ya ndege anaenda nje ya nchi, na kwamba manispaa inamtaka kufika kabla ya februari 7 mwaka huu.

Wakandarasi waliopitishwa na halmashauri zote mkoani Kagera wamesaini mikataba yenye jumla ya shilingi bilioni 6 milioni 172 na laki saba zilizotolewa na serikali kuu

Comments

Popular posts from this blog

Sera ya Viwanda iendane na mabadiliko ya soko la wakulima

Ziara ya Jaji Mkuu Zanzibar mhe. Omar Othman Makungu katika picha

Mrajisi ataka wananchi kufika mahakamani kutoa ushahidi