NSSF wawezesha huduma ya upimaji tezi dume kwa wanyonge Mtwara

Na Florence Sanawa
Sauti ya Mnyonge, Mtwara

MFUKO wa Hifadhi ya  Jamii (NSSF) umewakumbuka wanyonge Mkoani Mtwara kwakuwaleta madaktari zaidi ya 25 ambao watatoa huduma ya vipimo kwa magonjwa ya Tezi dume Kwa teknolojia Mpya, Kansa ya mlango wa kizazi, Kisukari, shinikizo la damu (Presha), kansa ya matiti.

Zoezi hilo litakaoendeshwa muda wa siku saba litajumuisha wanachama na wasio wanachama wa mfuko huo kwakutoa huduma hiyo bure.

Akizungumza wakati wa kuzindua huduma hiyo jana Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gellasius Byakanwa amesema kuwa wananchi wanapaswa wajitokeze ili kujua hali zao kiafya.

“Nimeona huduma zikitolewa za vipimo hii ni fursa kwa wakazi wa mtwara kufika na kujua hali zao ili kuboresha afya hatua ambayo itachangia kuongeza kasi ya uzalishaji mali katika mkoa wetu”

Nae Mkurugenzi Uendeshaji Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Bathow Mmuni alisema kuwa ujio wa madaktari hao ni sehemu ya kurudisha fadhila kwa wananchi kutokana na mafao na faida wanayopata kama mfuko huo wa hifadhi ya jamii.

Comments

Popular posts from this blog

Sera ya Viwanda iendane na mabadiliko ya soko la wakulima

Ziara ya Jaji Mkuu Zanzibar mhe. Omar Othman Makungu katika picha

Mrajisi ataka wananchi kufika mahakamani kutoa ushahidi