Vijana Zanzibar wapongeza kupatiwa wizara inayowahusu

Na Hajji Nassor
Sauti ya Mnyonge, Zanzibar

BARAZA la vijana wilaya ya Chakechake kisiwani Pemba, wamempongeza rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Mhe: Dk Ali Mohame Shein, kwa uamuzi wake wa kuwapandishi hadhi vijana, kwa kuwawekea wizara yao.

Walisema hatua hiyo ta rais, inaonesha jinsi anavyovutiwa na harakati na shughuli zao mbali mbali, na ndio maana akamua kuwapandisha hadhi kutoka kama Idara na sasa kuwepo na jina la wizara inayoonzai na vijana.

Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa baraza hilo, Hamad Bakar Hamad, wakati akifungua kongamano la vijana lililokuwa na lengo la kupinga mimba za umri mdogo na udhalilishaji, lililofanyika skuli ya Maandalizi Madungu.

Alisema, sasa kazi iliobakia kwa vijana nchini ni kuona wanaitumiaje wizara yao, kwa lengo la kujitafutia maendeleo, baada ya rais hivi karubuni kuanzisha wizara hiyo, inayijitegemea.

Alisema ndani ya wizara hiyo, inaweza vijana kuwaonyesha njia ya kufikia malengo yao, ikiwemo kuanzisha miradi miradi, ujasiriamali, kilimo, ufugaji na kuondokana na mawazo kwamba kila kijana lazima aajiriwe serikalini.

“Mimi nichukue nafasi hii kumpongeza sana raie wetu, kwa kutuwekea wizara yetu kamili, ambapo awali tulikuwa kama idara, lakini sasa ni nafasi yetu vijana kufikia malengo yetu,”alieleza.

Katika hatua nyengine Mwenyekiti huyo wa baraza la vijana wilaya ya Chakechake, alisema kila mmoja anawajibu wa kujilinda na mimba za umri mdogo, ili afikie malengo yao.

Mapema Afisa Ustawi wa Jamii wilaya ya Chakechake, Ali Mohamed Ali, alisema matend ya udhalilishaji yanafaa vijana wayaundie kamati, ili kuyapiga vita kutokana na kushamiri kwake.

Alisema katika siku za hivi karibuni amekuwa akipokea kesi kadhaa zinazohusu mvutano wa malezi ya watoto, ambapo baadhi yao huishia kwenye kukosa haki yao ya elimu na kuingia katika makundi maovu.

Kwa upande wake Afisa Vijana Zanzibar Salma Hairalla, amesema kampeni hiyo ni ya mwanzo, na wanatarajia kuwafikia zaidi ya vijana 1000 kuwapa elimu hiyo.

Alisema kila wilaya itafanyiwa kongamano la siku moja la muda mfupi, ili kuwapa elimu ua jinsia vijana, kwa lengo la kujikinga na majanga yaliowazunguruka ikiwa ni pamoja na mimba za umri mdogo.

“Baada ya kampeni hii, tunataka kuona vijana wamebadilika hasa kuondokana kwa wale wanawake, kupata mimba kabla ya wakati, na kutokuwepo kwa udhalilishaji ndani ya jamii za Zanzibar,”alieleza.

Baadhi ya washiriki wa kongamani hilo, walisema chanzo cha kuwepo kwa udhalilishaji ni kwa wazazi na walezi kusahau wajibu wao, wa kimalezi kwa watoto.

Ali Is-mail wa shehia ya Tibirinzi, alisema wapo wazazi wamekuwa wakitoa uhuru mkubwa kwa watoto, bila ya kujali madhara ambayo anaweza kuyapata ikiwa ni pamoja na mimba kabla ya wakati wake.

Nae Rukia Hasnuu wa Chonga, alisema wapoa vijana ambao hawajajielewa nini wanafanya na malengo yao ya baadae, na ndio maana hujitokeza ndoa na mimba zisizotarajiwa.

Katika hatua nyengine mjumbe wa baraza la vijana shehia ya Wara Maryam Juma Bakari, alisema elimu ya jinsia bado inahitika kwa vijana waliowengi, ili kuwakinga na udhalilishaji.

Kongamano hilo la siku moja lililowashirikisha vijana zaidi ya 100 kutoka  wilaya ya Chakechake, ni mfululizo wa elimu inayotolewa ba serikali, kwa vijana ili kuwaelekeza kwenye maadili na njia mwafaka kwa ajili ya maisha yao na taifa.

Comments

Popular posts from this blog

Wananchi wajenga wodi baada ya kuchoshwa na kujifungulia sakafuni

Sita wapotea katika mazingira tatanishi wilayani Wete

Jaji Mkuu Zanzibar awashukia mahakimu wanaonyanyasa watuhumiwa