Uvuvi haramu wasababisha Mtwara kutegemea samaki toka Msumbiji

Na Mwandishi Wetu,
Sauti ya Mnyonge, Mtwara

Kutokana na baadhi ya wavuvi kutumia zana haramu kuvua samaki katika bahari ya Hindi kumesababisha wikazi wa wilaya ya Mtwara kutegemea kitoweo cha samaki kutoka nchi jirani ya Msumbiji.

Kutokana na athari hizo wananchi wanaoish pembezoni mwa bahari ya Hindi wametakiwa kilinda na kuwafichua wote wanaodhoofisha juhudi zinazofanywa na serikali pamoja wadau mbalimbali za kuhifadhi mazao ya bahari kwa kutoa taarifa kwa vyombo vya ulinzi na usalama.

Wito huo umetolewa na mkuu wa wilaya ya Mtwara ,Evod Mmanda wakati wa ufunguzi wa mafunzo maalumu kwa wawakilishi wa mtandao wa ulinzi wa rasilimali za bahari (BMU) unaojishughulisha kuratibu utekelezaji wa shughuli mbalimbali za usimamizi wa raslilali za bahari ulioandaliwa na Shirikishi Maendeleo ya Jamii (WWF)

Insert…Evodi Mmanda-mkuu wa wilaya ya Mtwara

Kwa upande wake afisa usimamizi shirikishi raslimali za uvuvi wa shirikishi wa WWF,Geofrey Kamugisha amesema lengo la  kuanzishwa kwa vikundi vya usimamizi wa rasilimali za uvuvi ni kutokana na kukosekana kwa chombo kilichokuwa kinaratibu shughuli hizo.

Mwenyekiti wa mtandao wa BMU wilaya ya Mtwara Shabani mayonzi amedai kuwa katika kusaidia sekta ya uvuvi wanakabiliwa na changamoto ya kupata vitisho kutoka kwa wavuvi kwa kuonekana  wanahatarisha maisha ya wanaojihusish na uvuvi haramu.

Comments

Popular posts from this blog

Sera ya Viwanda iendane na mabadiliko ya soko la wakulima

Ziara ya Jaji Mkuu Zanzibar mhe. Omar Othman Makungu katika picha

Mrajisi ataka wananchi kufika mahakamani kutoa ushahidi