Mitego ya panya inavyomnufaisha mzee Mpupua kwa miaka 36
Na, Florence Sanawa
Sauti ya Mnyonge, Mtwara
Mzee Edger Martin Mpupua afurahishawa na biashara ya kuuza panya wilayani masasi huku akidumu kwa kutengeneza mitego ya hicho kwa zaidi ya miaka 36.
Anasema kuwa utengenezaji wa mitego hiyo umekuwa ukibadilika kila wakati hali ambayo inapelekea bei yake kupanda kutokana na mahitaji ya panya kuwa makubwa ambapo awali ilikuwa ikiuzwa kwa shilingi 200 hadi kufikia shilingi 1000.
Soko kubwa la panya liko katika maeneo ya Mtandi, Migongo, Mwimbaka, Mbarika na Kanyimbi ambapo ndio kuna wateja wengi wa bidhaa hiyo ambayo huuzwa kwa mafungu watano kwa shilingi 500 na tunafunga 8 kwa shilingi 1000 ambao ni wakubwa kwa siku unaweza kuvuna zaidi ya panya 2000 kwa siku.
“Kihistoria uhaba wa samaki ndio ulitufanya tuanze kutega panya kama kitoweo wanatusaidia kwakuwa hawana msimu ingawa kuwawinda napata shida hasa wengi wetu tunatembea peku hata wenye viatu wamekuwa wakitumia viatu ambayo bado vinawafanya wawe kwenye hatari zaidi ya kukutana na nyoka na wanyama wengine…..
“Nilianza kutengeneza mitego mwaka 1982 ambapo nilikuwa nauza mmoja hiyo hata maisha yangu naendesha kwa biashara hiyo, mara nyingi tunakwenda porini tunawavuna kisha tunawakausha kwa moto na kuwauza kwa mafungu hicho ni chakula chetu ambalo kila mara hutumia nimekuwa nikimaliza mipango midogo midogo ya kifamilia kwa kuuza panya na mambo yamekuwa yakienda sawa” alisema Mpupua
Comments
Post a Comment