Mbunge aomba fedha za maji kwa wananchi wa Tandahimba
Na Mwandishi Wetu
Sauti ya Mnyonge, Tandahimba - Mtwara
Kutokana na wananchi wa wilaya ya Tandahimba mkoani Mtwara kukosa huduma ya maji, mbunge wa Tandahimba, Katani Katani ameiomba serikali kuharakisha mchakato wa kuipatia fedha mamlaka ya maji wilaya humo Makonde ,ili kutatua kero hiyo.
Takwimu za mkoa zinaonyesha wilaya ya Tandahimba ni asilimia 24 pekee ya wakazi wake wanaopata huduma ya maji baada ya mradi wa Makonde vifaa vyake kuchakaa na kukosekana kwa umeme wa uhakika licha ya kuwa na mtandao wa maji.
Pia, Katani amewataka wananchi kujitokeza kutoa maoni kwa tume itakayopita wilayani humo kupata maoni juu ya uundwaji wa mamlaka ya maji ili kusaidia kupata idadi kubwa ya watu na kuifanya wizara ya maji kuona hitaji la wanatandahimba.
“Maji ndio kila kitu, bila maji huwezi kuwaza shughuli nyingine za maendeleo ipasavyo,hivyo nawasihi wanatandahimba mjitokezee kwa wingi kutoa maoni juu ya uundwaji wa mamlaka ya maji,maana najuwa lazima watapita kupata maoni toka kwenu,tukipata mamlaka ya maji tutapunguza tatizo kwa asilimia themenini na mbili”amesema katani
Kukosekana kwa maji wilayani humo hali hiyo imedumu kwa muda mrefu na kusababisha huduma mbalimbali za kijamii kushindwa kufanyika kwa ufanisi,huku wananchi uona maji ni miongoni mwa anasa kutoka na upatikanaji wake kuwa wa shida nap engine kununua kwa bei ya kuanzia shilingi mia tano mpaka elfu moja kwa ujazo wa lita ishirini.
Akizungumza na gazeti hili mhandisi wa maji wilayani humo, Peter Malekia amekiri kuwepo kwa tatizo hilo kwa muda mrefu licha ya mradi wa maji wa Makonde kuwa na uwezo wa kusambaza mkoa mzima wa Mtwara.
“Hali ya upatikanaji wa maji ni mbaya sana kupita wakati wowote ule”amesema mhandisi Malekia
Aidha amesema tatizo hilo linachangiwa na changamoto mbalimbali ikiwepo uchakavu wa miundombinu, kukosekana kwa umeme wa uhakika na kupasuka kwa mabomba.
Changamoto nyingine ni upungufu wa matanki ya kusambazia maji na kwamba wizara kwa kushikiana na mamlaka ya maji Makonde imeanza kufanyia matengenezo mashine zilizopo katika kituo hicho pamoja na wizara kuahidi kupeleka fedha mwisho wa mwezi Machi kwaajili ya uakarabati wa mitambo.

Comments
Post a Comment