Profesa Kitila Mkumbo ashusha neema ya maji kwa wanyonge mkoani Lindi

Na, Haika Kimaro
Sauti ya Mnyonge, Lindi

ZAIDI ya asilimia 57 ya wakazi wa mji wa Lindi wataanza kupata huduma ya maji safi na salama kuanzia leo baada ya mradi wa maji wa Ng’apa uliokuwa ukisua sua katika utekelezaji wake kuonyesha kukamilika kwa asilimia 80.

Kukamilika kwa mradi huo ambao umegharimu zaidi ya Sh bilioni 35 utanufaisha wakazi wa mji wa Lindi wote ambao tayari walishaunganishiwa mfumo wa maji pamoja na kuendelea kuunganisha wateja wapya .

Hayo yameelezwa na katibu mkuu wizara ya maji, Profesa Kitila Mkumbo alipotembelea mradi huo kuona maendeleo yake ambapo pia amempa mkandarasi anayeutekeleza mwezi mmoja kuukamilisha badala ya tarehe 15 kama ilivyokuwa awali.


Mhandisi wa mamlaka ya maji  safi na taka (Mtwara) Mtuwasa  aliyekabidiwa kusimamia mradi huo baada ya uongozi wa Mamlaka ya maji Lindi(Luwasa) kushindwa,Mhandisi Mashaka Sitta  anasema miundombinu ya kufikishia wananchi maji tayari imekamilia.


Comments

Popular posts from this blog

Sera ya Viwanda iendane na mabadiliko ya soko la wakulima

Ziara ya Jaji Mkuu Zanzibar mhe. Omar Othman Makungu katika picha

Mrajisi ataka wananchi kufika mahakamani kutoa ushahidi