Ukosefu wa maji salama wawatia hofu wananchi kijiji cha Msakala

Wananchi wa kijiji cha Msakala kata ya ziwani katika halmashauri ya wilaya ya Mtwara, wanalazimika kutumia maji ya bwawa kwa matumizi ya nyumbani kutokana na kukosekana kwa maji safi na salama na hivyo kuhatarisha afya zao. Kijiji cha Msakala ni moja kati ya vijiji vinavyounda kata ya Ziwani yenye jumla ya wakazi 8,919 kwa mujibu wa sesnsa ya watu na makazi ya mwaka 2012. Akizungumza mkazi wa kijiji hicho Mwajuma Mbango amesema wanalazimika kutmia maji hayo na kuhatarisha maihsa yao kwani hawana mbadala.  
Mwajuma Mbago, mkazi wa Ziwani, akiongelea kadhia ya maji wanayoipata kijijini kwao 

Kata hiyo ina chanzo cha maji lakini hakinufaishi wananchi na badala yake kinanufaisha kata nyingine ya Msangamkuuambapo mwenyekiti wa kijiji cha Msakala lilipo bwawa hilo Salum Majandika anaeleza hatua alizochukua katika kuwasaidia wananchi wake.

   
Salum Majandika, mwenyekiti wa kijiji cha Msakala, akiongea na Sauti ya Mnyonge 

Baada ya malalamiko hayo ya wananchi, nini kauli ya serikali juu ya kutatua changamoto hiyo, hapa mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Mtwara Omary Kipanga anaeleza. Kata ya Ziwani inaundwa na vijiji Vinne, ambavyo ni Msakala, Nambeleketela, Majengo na Mnawene

Comments

Popular posts from this blog

Sera ya Viwanda iendane na mabadiliko ya soko la wakulima

Ziara ya Jaji Mkuu Zanzibar mhe. Omar Othman Makungu katika picha

Mrajisi ataka wananchi kufika mahakamani kutoa ushahidi