Dk. Shein afungua soko akisema wasioona maendeleo yaliofanywa wapimwe akili
Na, Haji Nassoro
Sauti ya Mnyonge, Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein, amewataka wananchi kisiwani Pemba, kuwabeza na kukjitenga nao, mbali watu wanaosema tokea Mapindizi ya mwaka 1964 hakujafanywa jambo, na wanahitaja kupima akili zao.
Alisema, inawezekana wapo wanaopita pita wakielezea kuwa hakuna maendeleo yaliofaikiwa hapa Zanzibar, licha kuwa wanaosema hivyo, wamesoma na kuzaliwa ndani ya nchi hii.
Dk Shein, ameeleza hayo muda mfupi, baada ya kulifungua rasmi soko jipya lililopo Tibirinzi mjini Chakechake, ikiwa shamra shamra za miaka 54 ya mapinduzi Zanzibar.
Alisema, kutokana na maendeleo yaliopo, kama wakitokezea wanaobeza mafanikio yaliopo, sharti watazamawe mara mbili, na ikiwezekana wapimwe akili zao.
Kuhusu soko alilolifungua, alilitaka Baraza la Mji Chakechake, wasijelifanya sehemu ya kuwabagua wananchi kiajira, na kupatiwa vikuta, maana dhana hiyo ilishazikwa mara tua baada ya mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964.
“Soko hili ni la watu wote, awe CUF, CHADEMA au CCM na vyama vyengine, sasa sitaki patokezee mtu kabaguliwa kwa ajira, ununuzi ua uuzaji kwa sababu ya itiakadi yake”,alisema.
Aidha dk Shein alitumia nafasi hiyo, kuwakumbusha vijana kuwa, malengo makuu ya Mapinduzi ya Zanzibar ni kuwapatia wananchi huduma kadhaa bila ya malipo, ikiwa ni elimu, matibabu na ardhi sasa kuwa mali ya serikali.
Katika hatua nyengine rais huyo wa Zanzibar, aliutaka uongozi wa soko hilo, kujipanga kimkakati kuhakikisha uzuri na haiba yake, haipotei.
Alisema soko ambalo kwa Zanzibar kihuduma ni pekee, na lazima suala la kulitunza na kulienzi liwe ndio jambo la kwanza, ili na wengine waje wawahi kulitumia.
Akisoma risala ya kitaalamu, Katibu Mkuu wizara Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Joseph Abdalla Meza, alisema ujenzi huo wa soko la ghorofa moja, ulioanza mwezi April mwaka 2016, umetumia shilingi zaidi ya milioni 972.
Alieleza kuwa, fedha hizo ni kwa ufadhili wa benki ya maendeleo ya Afrika ADB, Shirika la chakula duniani IFAD, sambamba na serikali zote mbili za Tanzania.
Huduma zilizomo ndani ya soko hilo, pamoja na chumba maaluma cha kuhifadhi kama saamaki na nyama, uzalisha wa barafu, matenki, chumba cha Meneja.
Comments
Post a Comment